HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 14, 2019

Serikali yawataka vijana kuchangamkia fursa kwenye kilimo

 Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa, akizindua  vitabu vinne vinavyohusu masuala ya kilimo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Donald Mmari na Mtafiti Repoa Lulu Qlan`g (katikati). (Na Mpiga Picha Wetu).
Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa, akizingumza katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa REPOA Dk. Donald Mmari akizungumza katika hafla hiyo.

NA MAKUBURI ALLY
SERIKALI imewaasa  vijana kuwekeza elimu zao katika katika sekta ya kilimo ili kuweza kutatua changamoto ya ajira ambayo imekuwa ni kilio kwa vijana wengi wakitanzania.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa vitabu vinne vilivyoandaliwa na Taasisi ya Repoa inayojihusisha na mambo ya utafiti ambavyo vimelenga maendeleo ya kilimo, Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa alisema vijana wanatakiwa wabadilike na wasome alama za nyakati hasa kutokana na mazao yaliyopo hapa nchini yanahitajika katika nchi za jirani ikiwemo Msumbiji, Malawi na mpaka nchi za Ulaya.
“Wakulima wetu wamekuwa wakizalisha mazao bila kujua wanauza wapi lakini ndani ya Serikali hadi sasa mtaona chini ya wizara ya kilimo kuna idara ya masoko kwaajili ya timu ya kutafuta masoko,” alisema Bashungwa.
Aidha, Bashungwa alisema kuwa unaweza ukawa kijana si lazima ukashike jembe unaweza ukaanzisha kampuni ambayo imejikita katika masoko ya mazao ya wakulima wa hapa nchini na ikawa ajira kwako.
Katika vitabu ambavyo vimezinduliwa na Naibu Waziri vimelenga kutoa elimu juu ya kilimo pamoja na umwagiliaji hasa kutokana na tafiti ambazo walizifanya Repoa.
Moja ya vitabu hivyo kimeelezea Elimu na uzalishaji kwenye kilimo Tanzania Vijijini, kimeandaliwa na Profesa Lucas Katera, kingine kimeeleza Tathmini ya mfumo wa Kitaasisi wa maboresho wa Utumishi kwa Umma, ambacho kimeandaliwa na Dk Jamal Msami, kingine kinazungumzia Mabadiliko ya kitaasisi na vikwazo vya Ushindani kwenye Masoko, ambacho kimeandaliwa na Dk Donald Mmari na kitabu ambacho kimezinguzia Sera za kilimo na jitihada za Kupunguza Umasikini Tanzania ambacho kimeandaliwa na Profesa Paschal Mihyo.

1 comment:

  1. Amazing! This blog looks just like my old one! It's on a entirely different subject but it has pretty much
    the same layout and design. Superb choice of colors!

    ReplyDelete

Pages