HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 12, 2020

Amshukuru Rais Magufuli ujenzi wa maabara

Mratibu wa Huduma za Maabara  Wilaya ya Kigamboni, Grace Maliva, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani.
 

Na Asha Mwakyonde

MRATIBU wa  Huduma za Maabara  Wilaya ya Kigamboni, Grace Maliva amemshukuru Rais  John Magufuli  kwa kuwezesha kupatikana Maabara kubwa tatu  za kisasa  katika wilaya  hiyo  kwa kipindi kifupi tangu mchakato wa ujenzi ulivyoanza.

Haya ameyasema  jijini Dar es Salaam Februari 11, 2020 mara baada ya Magufuli  kuzindua Wilaya  mpya ya Kigamboni pamoja na majengo ya maabara, Grace amesema serikali ya awamu ya tano imeweka kipaumbele  cha kujali afya  za Watanzania ambao ndio walipata kodi.

Mratibu huyo amesema upatikanaji wa maabara hizo zitarahisisha kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaohitaji vipimo na kwamba watahudumiwa kwa wakati pindi zitakapokamilika tofauti na hali ilivyo sasa.

Ameongeza kuwa awali hali ilikuwa mbaya kwani wilaya nzima yenye kata 67 ilikuwa na Maabara moja ambayo ni vijibweni na vyumba vilivyokuwa mfano wa Maabara vitatu.

Amefafanua kwamba maabara moja ipo  katika kituo  cha afya Kimbiji, kingine  kituo cha afya  cha Kigamboni na kwamba  kmoja io  Somagila Mjimwema ambapo ndio hospital ya wilaya.

"Mafanikio haya yanatokana jitihada zinazofanywa na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  kwa kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa na hii ni pamoja na ujenzi wa maabara, kama hizi na vifaa," amesema Grace.

Aidha amemshukuru Rais  Magufuli kwa kujali watumiaji wa majengo husika na kuwaweka kwenye kamati za ujenzi  na kuwa washauri wa karibu wa miundombinu inayojengwa hasa upande wa Maabara.

1 comment:

  1. Kazi nzuri sana ya serikali ya awamu ya tano lakini pia kwako Mratibu kwa kuweza kusimamia na kupata kulingana na viwango stahiki kwa lengo la kusaidia watanzania wenzetu.

    ReplyDelete

Pages