HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 12, 2021

HALMASHAURI YA WILAYA YA MULEBA YATOA MADAWATI 836 KWA SHULE ZA MSINGI 26

 


Na Lydia Lugakila, Muleba


Halimashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera imegawa madawati 836 katika shule za msingi  zipatazo 26 kupitia mapato yake ya ndani ambayo yamesaidia  kuondoa changamoto ya uhaba wa madawati shuleni.

Akigawa madawati hayo Mkurugenzi Mtendaji wa halimashauri ya Wilaya ya Muleba Bwana Emmanuel Sherembi amesema katika mwaka huu wa fedha halmashauri hiyo ilikuwa na mahitaji ya madawati 51,534 na kulikuwa na madawati 49,576 upungufu ukiwa ukiwa ni madawati 1948.

 sherembi amesema kuwa halmashauri ya Wilaya ya Muleba kupitia mapato yake ya ndani imetengeneza madawati 1,036 katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza madawati 200 yalitengenezwa na kusambazwa katika shule za msingi tisa.

Aidha Mkurugenzi huyo ameagiza walimu wakuu kuhakikisha wanakarabati madawati yote ndani ya siku saba kwani ofisi ya Mkurugenzi imetoa kibali cha utengenezaji wa madawati mabovu katika shule zilizoomba 58 ikiwa ni jumla ya madawati 1074 na hivyo kiumaliza kabisa changamoto ya madwati katika Wilaya hiyo.

Awali akisoma taarifa  kaimu afisa elimu msingi Wilaya ya Muleba Bi. Restuta Stephano amesema Wilaya ya Muleba ina jumla ya shule za msingi 241 ambapo shule 227 ni za serikali na shule 14 ni shule binafsi jumla yake wakiwa wanafunzi   154,604.

1 comment:

  1. Kwa niaba ya wakuu wa shule wilaya ya Muleba kwa dhati ya mioyo tunatoa shukurani na pongezi za dhati kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Muleba @⁨DC Mlb Eng. Richard Ruyango⁩ na Mkurugenzi Mtendaji @Emmanuel Shirembi kwa kutatua changamoto ya madawati katika wilaya yetu.

    Tunawapongeza kwa kazi nzuri iliyotukuka na zaidi tunawaahidi utumishi uliotukuka katika kuhakikisha tunaipandisha wilaya ya Muleba na mkoa wa Kagera juu kielimu👏👏

    *James V. Tarimo _(Mjoli wa Bwana)_*
    Mkuu wa Shule - Kyota

    ReplyDelete

Pages