Na Elizabeth John
KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa Nchini
(TPBC) imemtafutia bondia Francis Cheka mpambano wa marudiano kati yake
na bondia Chiotra Chimwemwe wa Malawi anayetokea katika jiji la Addis Ababa,
Ethiopia.
Mpambano huo wa kimataifa unatarajia
kufanyika Januari 26 mwakani, ambayo pia itakuwa ni siku ya ufunguzi wa mkutano
wa wakuu wa nchi za Africa (AU Summit) katika jiji hilo la Abesinia.
Cheka na Chimwemwe watakutana mjini
Arusha Desemba 26 (Boxing Day) katika mpambano wa kutafuta nani mbabe wa uzito
wa Super Middle katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi
(IBF AMEPG).
Katika mpambano huo mafahali hawa wawili wataumana kiume kwa raundi 12 za dakika tatu kwa kila raundi moja.
Mpambano wa Cheka na Chimwemwe
umeandaliwa na Kampuni ya Screen Hills (T) Investment ya Dar es Salaam
inayomilikiwa na promota maarufu aliyewahi kuwa bingwa wa taifa katika ngumi za
ridhaa na kulipwa Andrew George ‘Chagga Boy’.
Kwa mujibu wa Rais wa TPBC, Onesmo
Ngowi, umaarufu wa mabondia hao umewafanya mapromota wanaoandaa tamasha la
kuchangisha pesa kwa ajili ya kulisha watu wenye njaa katika bara la Afrika.
Mpambano huu umeidhinishwa na
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na Cheka kupewa kibali na Kamisheni ya
Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC).
No comments:
Post a Comment