HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 19, 2012

KUMNG'OA LIONEL MESSI BARCELONA PAUNI MIL. 312


Lionel Messi

BRCELONA, Hispania

Hivyo Man City - ambao ni mabingwa wa England na Chelsea waliovuliwa ubingwa wa Ulaya hivi karibu na kutupwa katika michuano ya Europa League, zitapaswa kuvunja benki kama zinahitaji saini ya nyota huyo anayevunja rekodi za soka kila uchao

KLABU mbili za Ligi Kuu ya England za Manchester City au Chelsea zilizowahi kuripotiwa kuwania saini ya mshambuliaji Lionel Messi, sasa zitalazimika kuvunja benki na kulipa dau la pauni milioni 312 kumpata.

Mwanasoka Bora huyo kwa mwaka wa tatu mfululizo amekubakli kurefusha mkataba kwa miaka sita zaidi akiwa na klabu yake ya FC Barcelona wenye thamani ya pauni milioni 17 kwa mwaka, unaofikia tamati mwaka 2018.
Mshahara huo unamfanya utamuwezesha kupata pauni milioni 102 katika kipindi chake cha mkataba na Barca, ambapo ukijumlisha na kipengele kinachomruhusu kuondoka klabuni Nou Camp kwa pauni milioni 210, inamfanya Messi kuwa na thamani ya pauni milioni 312 kwa sasa.

Hivyo Man City - ambao ni mabingwa wa England na Chelsea waliovuliwa ubingwa wa Ulaya hivi karibu na kutupwa katika michuano ya Europa League, zitapaswa kuvunja benki kama zinahitaji saini ya nyota huyo anayevunja rekodi za soka kila uchao, huku akiwa na nafasi kuibwa kutwaa tuzo ya nne ya Mwanasoka Bora wa Mawaka wa Fifa.

Ukiondoa kiwango cha pesa inayoweza kumuondoa Messi katika soka la England, imeelezwa na inajulikana uwapo wa nafasi finyu ya Messi, 25, kukubali kuihama Barca kuhamia klabu yoyote ya Ligi Kuu ya England.

Kiungo nyota wa klabu hiyo na mhimili mkuu wa mafanikio ya Barca, Xavi, 32, na nahodha mkongwe wa Carles Puyol, 34, nao pia wamekubali kurefusha mikataba yao ya kuendelea kukipiga Nou Camp.

Akizungumzia nyongeza za mikataba ya wakali hao, Mkurugenzi wa Barca Toni Freixa alisema: “Puyol, Messi na Xavi ni nguzo tatu za msingi. Ilikuwa jambo muhimu kuhakikisha tunabaki nao kwa kuwafunga na mikataba mipya.

“Ni uamuzi uliokuwa na baraka zote za Bodi ya Klabu, kufanya tulichofanya ili kuwabakisha Nou Camp ili kuendeleza programu kutokana na nyongeza zao,” alisema Freixa.

Kabla ya mkataba mpya, Messi alikuwa akilipwa mshahara wa pauni milioni 10 kwa mwaka, pamoja na asilimia 30 ambayo ilikuwa ikijumuishwa kutokana na kiwango chake dimbani kupanda, lakini mkataba huu utaigharimu zaidi na zaiodi Barca kutokana na sheria mpya za kodi za hapa.

No comments:

Post a Comment

Pages