Mkurugenzi
wa Prime Time, Joseph Kusaga makamu mwenyekiti wa Yanga, Clement
Sanga wakisaini mkataba katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya
klabu hiyo. Prime Time Promotion ilikabidhi hundi ya sh milioni 105 kwa
ajili ya kutumika katika mkutano mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika
Januari 19, mwakani
Mkurugenzi
wa Prime Time, Joseph Kusaga akifurahia jambo na Mwandishi wa michezo
wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Majuto Omary ambaye
pia ni mwenyekiti wa timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo,
Taswa FC mara baada ya kukamilika zoezi kusaini mkataba na klabu ya
Yanga kwa ajili ya kusimamia shughuli zao mbali mbali.Prime
Time Promotion ilikabidhi hundi ya sh milioni 105 kwa ajili ya kutumika
katika mkutano mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Januari 19,
mwakani
Mkurugenzi
wa Prime Time, Joseph Kusaga akikabidhi hundi ya sh milioni 105 kwa
makamu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga kwa ajili ya kutumika katika
mkutano mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Januari 19, mwakani.
DAR ES SALAAM, Tanzania
KAMPUNI ya Prime Time Promotion imeikabidhi mabingwa
wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga hundi ya shs Milioni 105 kwa ajili
ya kutumika katika mkutano wake mkuu wa mwaka wa wanachama uliopangwa kufanyika
Januari 19, mwakani.
Fedha hizo zilikabidhiwa katika mkutano maalum
uliowakutanisha viongozi wa Yanga na wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye Makao
Makuu ya klabu hiyo, Jangwani.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema
kuwa klabu yake imeingia makubaliano na Prime Time kwa kusimamia shughuli zake
zote ikiwa pamoja na mkutano huo.
Sanga alisema kuwa
mbali ya mkutano huo, Prime Time itakuwa na jukumu la kuandaa mechi
mbali mbali za kimataifa kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao na baadhi ya
malipo yatachukuliwa na kampuni hiyo.
Alisema kuwa hatua hiyi ni ya kuifanya klabu yao kuwa ya
kisasa zaidi na kutambua kampuni zenye uwezo wa kufanya shughuli mbali mbali
kama Prime Time Promotion kufanya kwa niaba yao.
“Kuna kampuni zenye uwezo au utaalam wa kufaya
matukio mbali mbali kama Prime Time ambazo zinatakiwa kupewa nafasi hiyo,
uongozi hauwezi kufanya shughuli zote, tunataka kuendesha klabu kisasa zaidi,”
alisema Sanga.
Naye Mkurugezi wa Prime Time Joseph Kusaga alisema
kuwa makubaliano hayo yatahusisha pia mechi ya kimataifa itakayofanyika Januari
12 na 13 na shughuli nyingine za klabu hiyo ili kuongeza kipato.
Kusaga alisema kuwa wamevutiwa na Yanga kutokana
uongozi wao kuongoza kwa uwazi zaidi na kuvutiwa hatua yao ya hivi karibuni ya
kuweka mapato na matumizi wazi kwa wanachama na wadau wa michezo kwa ujumla.
Alisema kuwa huu ni mwanzo tu kwani kwa mwaka 2013
wamejipanga kufanya kazi na vilabu vyote nchini ili kukuza na kuendeleza mchezo
huo. Kituo cha Televisheni cha Clouds kinatarajia kuonyesha live mkutano huo.
No comments:
Post a Comment