Na Mroki Mroki, Arusha
MAPOKEZI ya Kihistoria katika jiji la Arusha yamefanyika leo
wakati wafuasi, Mbunge wa Arusha Mjini kwa Tiketi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema walipo miminika kwa Wingi
kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) hadi katika Viwanja
vya Kilombero mjini hapa alipohutumia maelfu ya wana CHADEMA Arusha Mjini. SOMA
ZAIDI: www.mrokim.blogspot.com
Mapokezi hayo yamefanyika wakati Godbless Lema alipokuwa
akirejea mjini Arusha akitokea jijini Dar es Salaam kusikiliza hukumu ya Rufani
ya Keshi yake ya Kuvuliwa Ubunge iliyotolewa maamuzi ya kumrejeshea Ubunge wake
Desemba 21,2012.
Maelfu ya wananchi wakiwa katika msafara mrefu zaidi ya
pikipiki 500 na magari ulianzia Uwanja wa Ndege KIA mara baada ya Mbunge huyo
kuwasili uwanjanai hapo majira ya saa 4:20 Asubuhi.
Aidha Maandamano hayo ya Mapokezi ya Mbunge huyo, hayakuwa
na hata chembe ya Askari Polisi waliovalia sare wala magari yao ya diria kama
ilivyozoeleka na kuyafanya yafanyike kwa amani na utulivu katika maeneo yote
yaliyopita.
Huku wakiimba nyimbo za furaha hasa zile za “Oya oya Jembe
letu limerudi” Wanachadema hao walijigawa na baadhi kulinda amani huku wengine
wakiongoza magari.
Father Kidevu Blog ilishuhudua maelfu ya wakazi wa mji wa
Arusha wakiwa katika hali ya furaha na kusimama kando ya barabara kushuhudia
mapokezi ya Mbunge huyo.
“Haijawahji tokea hapa Arusha, kuwapo kwa msafara mrefu
namna hii wa mapokezi ya kiongozi yeyote Yule, tena yakiwa na amani ya kiasi
hiki,” alisikika akisema mmoja wa Watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.
Licha ya Kufanya mapokezi hayo na Kumshukuru Mungu kwa
Mbunge wao kurejea madarakani, lakini Wakazi wa Arusha na Wapigakura wa
Godbless Lema wamesema hivi sasa Mbunge huyo anapaswa kutulia na kutumia
kipindi kilicho baki cha miaka miwili ya madaraka yake kuwatumikia wananchi
katika kuhakikisha miradi ya Maendeleo inafanyika Jimboni humo na kuachana
kabisa na migomo na maandamano ya kila mara.
“Sasa Lema anatakiwa kututumikia wananchi maana sisi tumesha
mtumikia yeye vya kutosha kwa kuwa nae bega kwa bega katika kipindi chote cha
uongozi na hata alipokumbwa na msukosuko wa kuondolewa Ubunge, hivyo sasa ni
wakati muafaka wa yeye kuwaletea maendelea wana Arusha Mjini,” alisema Meshack Siriwa.
Godbless Lema alivuliwa Ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, 2012
mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika
hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM
waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo.
Wafuasi wa Lema wakishangilia barabarani wakati Mbunge huyo akipita.
Mbwembwe za waendesha pikipiki wengine ziliwashinda na kuanza kuanguaka.
Furaha hiyo ilikuwa kwa kilu aliye Mwanachadema
Skafu na vitru mbalimbali vilivyo na alama ya CHadema viliuzwa jijini Arusha kwa wingi.
Mke wa Mbunge Godbless Lema akiwa kwenye gari pamoja na mtoto wao wakati wa mapokezi hayo.
Lema Arusha anafananishwa na Barack Obama
Watu walining'inia katika magari bila hofu
Huyu na e'eti' alikua anachukua kumbukumbu za Video....
Lena akiwa nba Mbunge wa Arumeru Mashuari CHADEMA, Joshua Nasari.
No comments:
Post a Comment