Na Elizabeth John
MSHINDI wa Epiq Bongo Star Search (EBSS) mwaka jana, Walter
Chilambo amesema Watanzani wategemee vutu vizuri kutoka kwake kwamba yeye ni
msanii mwenye kipaji na hakupata ushindi huo kwa kubahatisha.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Walter alisema wasanii wengi ambao wanashinda BSS huwa wanapotea na hawaonekani
tena katika soko la muziki yeye anakujua kivingine anaomba mashabiki wa muziki
wakae mkao wa kula.
“Washindi wengi wa BSS wanaishia hewani, mimi naamini
nitakua tofauti sana kwani nimejipanga kuleta mabadiliko ya muziki kwa vijana
wa Tanzania kwa kupitia BSS,” alisema Walter.
Walter alisema kwasasa yupo katika hatua za mwisho za
uandaaji wa kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Siachi’ ambapo Jumatatu anatarajia kuutambulisha na kuusambaza katika vituo mbalimbali vya
redio.
Mbali na kibao hicho Walter yupo kwenye maandalizi ya
kuachia albamu yake ya kwanza ambayo bado hajaipatia jina, itakua na nyimbo
zaidi ya kumi.
“Naomba mashabiki wa bongo fleva wakae mkao wa kula, wimbo
wangu wa kwanza nitautambulisha Jumatatu na albamu itakua tayari mwishoni mwa
mwezi huu tuombe uzima kutoka kwa mwenyezi mungu ili wapenzi wangu mpate
burudani iliyoenda shule,” alisema Walter.
No comments:
Post a Comment