Mwezesheshaji wa PSPTB, Bakari Mohamed akielekeza watalaam wa ununuzi. (Picha zote na Bryceson Mathias)
Na Bryceson Mathias, Makole – Dodoma
BODI ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imwewaonya Watalaam wa Taalum hiyo wa Taasisi za Umma na Binafsi, Waachane na tabia ya kupanga mipango ya Utekelezaji wa Miradi bila kuwa na ukakika wa mafungu, wanaponunua Vifaa, Kazi za Ujenzi na Huduma, kwa sababu wananchi wamechoshwa na Umangimeza.
Onyo hilo lilitolewa jana na Mwezeshaji wa PSPTB Bw. Godfred Mbangi pichani katika Semina Elekezi ya siku tatu kwa Watalam hao inayoendele kwenye Hoteli ya 56 mkoani Dodoma kuhusu uandaaji wa Mbinu na Mipango ya ya Ununuzi, huku akiasa mipango hiyo iwe wazi ili wanasiasa wasiitumie vibaya Majukwani.
Akiwafundisha Washiriki kuhusu Mipango kama Chombo cha kupunguza gharama na hatua tatu za kupanga mipango ya ununuzi iliyohusisha Maafisa Ununuzi na Ugavi toka kwenye Taasisi za Umma, Halmashauri mbalimbali na za Binafsi (PPP) nchini Bw. Mbangi alisema,
“Unaweza kupanga vibaya Mpango wa ununuzi wa Ujenzi wa Mradi fulani kwa wananchi ambao mafungu yake unategemea kuyapata baada ya Miezi Sita au zaidi lakini wanasiasa wasijue hilo hatimae wakiinuka Majukwani hawasemi hadi zipatikane fedha ila hujigamba watajengewa jambo ambalo ni hatari.
“Wananchi walivyo na Hasira kutokana na kuchoshwa na Umangimeza na Ahadi zisizotekelezeka, hudhani wewe (Mnunuzi) ndiye unayekwamisha wasitibiwe, watoto wao wasisome, maji yasipatikane, Umeme waiupate, hivyo huanza kwa walio nacho, hivyo wakiona gari lako wanachoma”.alionya Mbangi.
Naye Mwezeshaji Bakari Mohamedi wa Mzunbe (Lecturer) akifundisha mipango ya utendaji huo katika Sekta za Umma (Public Sector) alisema,
“Umma unataka kuona Thamani ya fedha (Value for Money) na Kazi iliyofanywa vinalingana, siyo Zahanati inajengwe leo kesho nyufa zinaonekana hata mtu anaweza kupita, hilo hutaelewana na wananchi, wanaweza kukuchoma moto kwa sababu sasa watu hawataki kujenga nchi ya kufikirika”.alisema Bw. Mohamed.
Bw. Mohamedi aliongeza kwamba, kwa kuwa wananchi wanachoshwa na kero zinazowasibu ambazo hazipatiwi majibu ya kina, wamekuwa na usongo na kodi yao inayotumika kulipa mikopo ya Ujenzi wa Miradi mbalimbali inayoingiwa.
Aidha alitolea mfano wa Richmond ambayo mipango yake inadaiwa kutumia Quotation ya siku 10 badala ya siku 14, jambo alilosema kutokana na uelewa mpana walionao wanaamua kupamba na walionacho na watendaji walio katika sehemu za maamuzi, na kuonya kwamba ikifikia hapo, Madawani wanakuazimia na utapoteza kazi bila sababu, hivyo ni bora kuwa makini na kufanya mawasiliano na kupata ushauri na PPRA kwa kila hatua ya ununuzi.
No comments:
Post a Comment