Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MBUNGE wa Jimbo la Kibamba (CCM), Angellah Jasmine Kairuki ametoa ahadi ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Kibamba baada ya ile ya awali kuchomwa moto wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi 29 Oktoba 2025..jpeg)
Akizungumza wakati wa mkutano maalum wa CCM Kata ya Kibamba ambao uliambatana na sherehe ya kuwashukuru wajumbe kufuatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo mkuu uliopita, alisema amesikia kilio cha Kata na ameamua kuchangia kiwango hicho.
"Naahidi nitachangia Tsh.Milioni 10 ili mpate ofisi yenye stara" alisema mbunge Kairuki.
Hatua hiyo imefuata ombi la Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kibamba, Roberty Rashid 'Whitedent' alisema hivi sasa hawana ofisi baada ya ile ya awali kuchomwa moto na kwamba wamepata sehemu na ujenzi upo hatua ya msingi.
Ofisi hiyo iliteketezwa wakati huo sanjari na zile za Mtendaji wa Kata ya Kibamba na Serikali ya Mtaa.
Mbunge Kairuki alisema kuwa wakati ofisi za mtendaji na serikali za mtaa zinasubiri fungu kutoka halmashauri, atatoa malipo ya pango ili watendaji hao ngazi ya Kata na Mtaa wapate kutekeleza majukumu yao kwa wananchi ipasavyo.
Upande mwinyine mbunge Kairuki alihidi na ametekeleza ahadi ya ujenzi wa vivuko na ametoa TSh.Milioni 2.7 kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha Kwamatembezi na vile vinavyo unganisha Kidimu na Kibamba, Kididimuo vipo katika mchakato.
"Pia nitagharamia ununuzi wa mipira ya maji kule ambapo miundombinu (mitaro) ipo tayari lakini hakuna mipira" alisema mbunge Kairuki.
Pia wahisani wa Ahmadiya alisema kuwa wamejitolea kujenga kisima kila mtaa ili kukabiliana na adha ya upungufu na ukosefu wa maji katika baadhi ya maeneo.
Kairuki amewataka wananchi kujitoke za kwa wingi pindi atakapo anza ziara Kata ya Kibamba mwishoni mwa Februari 2026, akiwa na mawaziri tofauti.
"Nikianza ziara jitokeze kwa wingi ili muulize na mumwambie waziri husika changamoto zenu" alisema.
Alisema ziara na mawaziri ameishazifanya Kata ya Saranga na Mbezi akiwa na Waziri wa Maji Juma Awesu na sasa zamu ya Kibamba.
Diwani wa Kibamba na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo Kata ya Kibamba, Elisha Otaigo alisema halmashauri imetenga pesa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za mtendaji na serikali ya mtaa.
January 13, 2026
Home
Unlabelled
MBUNGE KAIRUKI ATOA MILIONI 10 UJENZI OFISI YA CCM KIBAMBA
MBUNGE KAIRUKI ATOA MILIONI 10 UJENZI OFISI YA CCM KIBAMBA
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.



No comments:
Post a Comment