KIKOSI cha Azam FC, kimemaliza mechi za hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mamlaka ya Mapato Uganda 'URA' na kutinga nusu fainali ya Mashindano ya NMB Mapinduzi Cup 2026, ambako huenda wakaumana na Wekundu wa Msimbazi Simba SC.
Kwa ushindi wa leo, Azam FC chini ya kocha Florent Ibenge, wamefikisha pointi saba, mbili juu ya Singida Black Stars, hivyo kuongoza Kundi A na Sasa ataumana na kinara wa Kundi B, ambaye anaweza kuwa Simba SC ambao usiku huu wanaumana na Fufuni SC ya Pemba.
.jpeg)
Aidha, Singida Black Stars walioshika nafasi ya pili katika Kundi A, watasubiri hadi kesho kujua mpinzani wao, ambako wanaweza kuwa Yanga SC ambao watashuka dimbani dhidi ya Wakusanya Kodi wa Tanzania 'TRA United. Yanga ya Mreno Pedro Goncalves watakuwa wakisaka sare tu ili kutinga nusu fainali.
Wakati huo huo, nyota wa URA ya Uganda, Otti Ronald alitangazwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Mwenye Nidhamu Zaidi 'NMB Most Discipline Player' wa mechi dhidi ya Azam FC na kutwaa kiasi cha Sh. 500,000 kutoka NMB, huku Japhet Kitambala wa Wana Lambalamba akiibuka Mchezaji Bora wa Mechi na kuzoa Sh. Mil. 1.
January 05, 2026
Home
Unlabelled
Azam FC kuivaa Simba nusu fainali NMB Mapinduzi Cup?
Azam FC kuivaa Simba nusu fainali NMB Mapinduzi Cup?
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.



No comments:
Post a Comment