DAR ES SALAAM, Tanzania
BAADHI ya askari polisi wa vyeo vya chini
wamelalamikia vitendo vya ubaguzi vinavyofanywa
na uongozi wa juu wa Jeshi hilo, hususan katika
kusafirisha miili ya marehemu wa vyeo
hivyo vya chini.
Malalamiko hayo yametolewa kwa nyakati tofauti na baadhi ya polisi hao wa vyeo vya chini walipozungumza na mwandishi wa mtandao huu.
Kwa mujibu wa sheria na kanuni za jeshi hilo (PGO), inapotokea
askari yoyote amepoteza maisha bila kujali cheo chake, jeshi linapaswa
kutoa sh milion moja pamoja na sanduku
kwa ajili ya mazishi.
Walisema utaratibu huo wa PGO bado unaendelea kutumika na haujabadilika, lakini uongozi wa jeshi hilo, umekuwa ukitumia
ubaguzi katika kutoa msaada huo hususan kwa kuangalia vyeo.
“Ndani ya jeshi la polisi, askari anayefanya kazi
kubwa ni askari wa cheo cha chini yani Kostebo, Koplo na Sajenti lakini amekuwa
akidharauliwa na kutothaminiwa ukilinganisha na askari wenye vyeo ”kilalamika chanzo hicho.
Kikifafanua zaidi, chanzo hicho kilisema anapofariki
askari wa cheo cha chini kama Konstebo, Koplo, Sajenti na Meja wa Jeshi hilo
wanatoa gari ndogo (Defender), kwa ajili ya kusafirishia familia ya askari huyo
hadi kwao kitendo ambacho kinakwenda kinyume na taratibu za jeshi hilo.
Hata hivyo, inapotokea kifo cha askari wa cheo cha
juu kuanzia nyota moja jeshi hilo linatoa gari lenye uwezo wa kuchukua watu 30 (Costa),
hali inayoleta mkang’anyiko.
“Askari hao wa vyeo chini wanajiuliza kuwa hivi askari
anayetambulika ni askari wa kuanzia nyota moja na kuendelea, huku sisi tukiwa
kama tambala la kupigia deki, tunajua kila tunachosema wanakikanusha japo ndiyo
ukweli wenyewe”kilieleza.
Alipoulizwa msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso
kuhusu malalamiko hayo, alisema inaoneka askari hao hawazifahamu vema taratibu
za serikali.
Alisema ni vema askari hao wakawauliza viongozi
wao kile wasichokijua ili waweze kupatiwa
ufafanunuzi kuliko kukimbilia kwenye vyombo vya habari kwani havitawasaidia
kutatua kile wasichokijua kuhusu taratibu za jeshi lao.
No comments:
Post a Comment