HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 20, 2013

MAHAFALI YA WANAFUNZI WA KIISLAMU JITEGEMEE SEKONDARI



  Mbunge wa Wawi kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) Hamadi Rashid Mohamed, akizungumza na wahitimu wa kidato cha sita wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari Jitegemee (JIMSA) ya jijini Dar es Salaam jana wakati wa mahafali yao ya 9 tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ambapo jumla ya wanafunzi 42 wamehitimu masomo yao wakiwa wanaume 26 na wanawake 16, kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Bakwata Taifa Rajab Alqushairiyyu na katibu Omary Msinzia.
  Baadhi ya wahitimu wakike wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwenye mahafali hayo.
 Baadhi ya wahitimu wakiume wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.
  Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohamed akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu hao wakiislamu wa shule ya sekondari Jitegemee mara baada ya mahafali yao yaliyoandaliwa na Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu ya shule hiyo.

Changamoto zinazowakabili zilizoelezwa kwenye risala ya wanafunzi hao

 Ni ukosefu wa mwalimu rasmi kwa somo la Islamic Knowledge,
Kutoruhusiwa kuvaa hijabu ingawa shule zingine za Jeshi hilo kama Makongo na Airwing wanaruhusiwa kuvaa lakini Jitegemee imekuwa vigumu kuruhusu pamoja na aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi na Usalama Abdurahmani Shimbo kwenye mahafali kama hayo alitoa agizo kuwa wanafunzi wakiislamu waruhusiwe kuvaa hijabu lakini agizo hilo halijatekelezwa.
 
 Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu Jitegemee (JIMSA) ilianzishwa 2004 ikiwa na Jumla ya wanachama 80 mpaka hivisasa inawanachama 233. Kati ya hao wanaume ni 185 na wanawake ni 48 na maustadh wanaofundisha dini kwa siku ya alhamisi sita.

No comments:

Post a Comment

Pages