Na Elizabeth John
BAADA ya kimya cha muda mrefu, msanii wa muziki kizazi
kipya, Pancras Ndaki Charles ‘PNC’, ameibuka na kusema amerudi kufanya mageuzi
makubwa katika muziki huo na kumtaka msanii mwenzake Naseeb Abdul ‘Diamond
Platinum’ ajiandae kuvaa vumbi.
Akizungumza na Habari Mseto Blog,
PNC, amesema kuwa ukimya wake haukuwa bure bali alikuwa anajipanga vema na ujio wake
mpya umekuja huku Diamond akioneka kuliteka anga la muziki huo na kumtambia
kuwa muda si mrefu atamfunika.
“Nilikaa kimya muda mrefu baada ya kutamba na ngoma yangu
ya ‘Mbona’ niliyomshirikisha Mr Blue, na kipindi chote nilikuwa najaribu
kuangalia jinsi nitakavyoliteka anga la muziki huu, na ujio wangu mpya umekuja
wakati Diamond akiwa safi, hivyo asubiri kuvaa vumbi kwani nitampoteza vibaya,”
alisema PNC.
PNC anayesimamiwa na meneja wake makini, Ostaz Juma, chini
ya lebo ya Mtanashati Entertainment, alisema hivi karibuni anatarajia kuachia ngoma
yake mpya ambayo hajataka kuitaja jina kutokana na maharamia waliopo katika
tasnia hiyo.
Mmsanii huyo ambaye ndiye kiongonzi wa kundi la Mtanashati
Entertainment, anawaomba wadau na mashabiki wa muziki huo kukaa mkao wa kula
kwaajili ya kuzipokea kazi zao zinazokuja.
No comments:
Post a Comment