LOME, Togo
TOGO imethibitisha kuwa
mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Emmanuel Adebayor amebadili
msimamo wake wa awali na sasa atakuwa sehemu ya nyota wa nchi hiyo wakaocheza
fainali za Mataifa Afrika baadaye mwezi huu.
Adebayor, 28, nyota
anayekipiga na klabu ya Tottenham, awali alikana kushiriki fainali hizo
zinazoanza Januari 19 huko nchini Afrika Kusini, lakini mazungumzo yake na Rais
wa Togo yamembadili msimamo.
Taarifa juu ya habari hii
zimeongeza kuwa, mshambuliaji huyo ataungana na kikosi chake nchini Ghana,
ambako kutakuwa na kambi fupi ya maandalizi ya mwisho mwisho ya timu hiyo
maarufu kama ‘Hawks.’
Rais wa Shirikisho la Soka la
Togo, Ameyi Gabriel, alisema: “Bila shaka tutakuwa katika michuano ya Mtaifa
Afrika tukiwa na Adebayor, tutakuwa sote pamoja nchini Afrika Kusini.
“Ni jambo muhimu mno kwamba
tutakuwa huko tukiwa naye kikosini, kwa sababu yeye ni mchezaji wetu na ni
nahodha wa timu.”
Ingawa Adebayor ameifungia Spurs
mabao matatu tu mwaka huu, uamuzi huu umetajwa kuweza kuiathiri klabu hiyo ya
jijini London, ambayo itapaswa kumtegemea mshambuliaji Jermain Defoe pekee.
Kama Togo itaweza kutinga
fainali za michuano hii, Adebayor anatarajia atakosa mechi nne za Tottenham,
lakini anaweza kurejea mapema kupigania klabu yake kwa sababu kikosi chake
kimepangwa kundi la kifo pamoja na Ivory Coast, Tunisia na Algeria.
No comments:
Post a Comment