Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa wakuu wa klabu ya Simba akimkabidhi Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga vifaa kwa ajili ya raundi ya pili ya ligi kuu inayoanza kesho. (Picha: Executive Solutions)
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa wakuu wa klabu ya Yanga akimkabidhi Msemaji wa Yanga, Lawrence Mwalusako vifaa kwa ajili ya raundi ya pili ya ligi kuu inayoanza kesho. (Picha: Executive Solutions)
DAR ES SALAAM, Tanzania
DAR ES SALAAM, Tanzania
Ikiwa
ni sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi vifaa
vya michezo kwa klabu maarufu za Simba SC na Young Africans SC kwa ajili ya awamu
ya pili ya msimu wa 2012/13 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki
hii.
Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema “Bila shaka Simba
na Yanga ndio klabu kubwa zaidi hapa Tanzania zikiwa kwa pamoja zimeweza kupata
mafanikio makubwa kwa kipindi kirefu na bado zinaendelea kufanya vizuri.
Tunajivunia kuweza kuziunga mkono klabu hizi katika jitihada za kuwania taji la ligi kuu msimu huu.
Vifaa
ambavyo leo tunatoa ni pamoja na mipira, viatu, soksi, shin guards, nguo za
mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vitu vingine vingi ambavyo vitawezesha timu
hizi za Simba na Yanga kucheza wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa hali ya
juu.
Kilimanjaro
Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji kinachoongoza
katika udhamini wa soka hapa nchini tunadhani kwamba uhusiano wetu na klabu
hizi ni kiungo muhimu sana katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania.
Tutaendelea kutimiza majukumu yetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu,
tutahakikisha tunalifikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio. kabisa kwani, pamoja na uhusiano huo mzuri na
klabu hizi mafanikio makubwa yanatarajiwa katika kuendeleza soka la Tanzania.
Kavishe
alisema kuwa ushirikiano kati ya Kilimanjaro Premium Lager na klabu hizo
umesimamia katika misingi ya kufanya kazi pamoja, uadilifu na kuendelea kupata
mafanikio. “Ushirikiano huu unasaidia kukuza mpira wa Tanzania, kuleta
msisimko, na kuvutia mashabiki wengi wa mpira wakati na vilevile kuwaweka
wachezaji wa Tanzania katika nafasi nzuri ya kimataifa.
Tunachukua
nafasi hii kuwashukuru viongozi wa Simba na Yanga walioko hapa, mashabiki wote,
vyombo vya habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano mzuri tunaoendelea
kupata kwenye udhamini wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio ya uhusiano wetu na
klabu hizi mbili maarufu.
“Tunaahidi
ushirikiano kwa klabu hizi nzuri na kama tunavyosema kila mara lengo letu ni
kufikisha mpira wa Tanzania kwenye ngazi za kimataifa na kuwafikisha mashabiki
wa mpira na wapenzi wa Kilimanjaro Premium Lager kwenye kilele cha mafanikio.”
No comments:
Post a Comment