HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

October 18, 2026

WANATAALUMA WATOA WITO KWA VIJANA

WANATAALUMA wamewataka vijana nchini kuenzi mila na desturi zenye kujenga jamii, huku wakishiriki kikamilifu katika kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

 Wito huo umetolewa katika Kongamano la Tano la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Katika kongamano hilo, Profesa Kalafunja Osaki aliwataka vijana kuzingatia maadili na kuepuka kuiga mienendo isiyo na manufaa kwa taifa.

Naye Profesa Joel Norbert alisisitiza umuhimu wa kulinda mazingira ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi


Akizindua kitabu chenye mkusanyiko wa makala za kitaaluma, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Haruni Mapesa, aliwahimiza Watanzania kutumia vitabu na matokeo ya tafiti kama chanzo cha maarifa na maendeleo.



 

No comments:

Post a Comment

Pages