Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Dkt.Mwasse ametaja mafanikio mengine kuwa ni kuongezeka kwa watumishi kutoka 111 hadi karibu 800, kuingia mikataba minne ya ubia katika miradi ya madini ya kimkakati na kuendelea kuboresha mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira, mkoani Songwe.
Ameongeza kuwa mchakato wa kuanzisha Benki ya Wachimbaji Tanzania umeanza kwa kushirikiana na wadau, kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa wachimbaji wadogo.
Amesisitiza kuwa STAMICO ni mwekezaji katika sekta ya madini, si mdhibiti, jukumu linalotekelezwa na taasisi husika za Serikali.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema mafanikio ya STAMICO yanaonyesha umuhimu wa mageuzi katika taasisi za umma, huku akisisitiza haja ya kuimarisha utafiti na ukusanyaji wa takwimu za kisasa ili kupima matokeo ya shughuli zake kwa usahihi.
STAMICO, ilianzishwa mwaka 1972 na inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100,inashiriki katika mnyororo wa thamani wa madini kuanzia utafiti na uchimbaji hadi uchenjuaji, uongezaji thamani na biashara ya madini.






No comments:
Post a Comment