HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 23, 2013

YANGA KUSHUKA DIMBANI LEO DHIDI YA BLACK LEOPARDS

Mashabiki wa yanga je watacheka leo katika pambano lao dhidi ya Black Leopards ya Afrika ya Kusini.
Na Mwandishi Wetu
KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga, Ernest Brandts amesema timmu yake itafanya vizuri katika mechi ya marudiano ya kirafiki dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini niliyopangwa kufanyika leo jijini Mwanza.
Brandts amesema kuwa wachezaji wake wote wamefikia kiwango kile anachotaka na mchezo huo utakuwa muhimu sana kwake kwani ni wa mwisho kabla ya kuingia katika kampeni za kutwaa  ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
"Black Leopards ni timu nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.
Ni mechi nzuri ambayo nadhani itakuwa ni kipimo kikubwa kabla ya kuanza kwa LigiKuu ya Tanzania Bara, wachezaji wangu wana viwango  vizuri sana kwa sasa na naamini makosa yaliyofanyika katika mechi ya kwanza hawatayafanya tena,” alisema Brandts.
Kuhusiana na mabacha wawili, Mbuyu Twite na Kabanga Twite  kucheza upande wa kulia, Brandts alisema kuwa wachezaji hao wana uwezo wa kucheza nafasi nyingi katika timu yake na uamuzi huo ulikuwa na faida kwa Yanga.
“Kabanga anauwezo wa kucheza nafasi ya ushambuliaji, katikati, beki zote na hata Mbuyu ana uwezo huo, hivyo uwepo wao katika timu ni mkubwa, niliwapumzisha kutokana na mipango ya mechi na wala si vinginevyo,” alisema.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pia wameamua kuicheza ili kuwapa burudani mashabiki wa Mwanza.
Kizuguto alisema kuwa Yanga haitakuwa na mechi yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya ziwa na hiyo ndiyo nafasi yao ya kuwapa waonyesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa Mwanza nini wamekipata kutoka Uturuki.
“Tuna mashabiki wengi sana Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu kwani mahsbaiki na wanachama watapata fursa ya kuona kiwango na maandalizi ya timu yao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili,” alisema Kizuguto.

No comments:

Post a Comment

Pages