Na Bryceson Mathias, Vumila Kilindi
KAMPUNI ya Udalali ya Jupitor Auction Mart ya Korogwe imetuhumiwa kutumia Jina la Rais Jakaya Kikwete kuvunja nyumba ya Meleji Salunge (39) wa Kitongoji cha Vumila, Kata ya Kinde Kilindi (W) na kuacha ya Juma Nassoro, huku wakidaiwa kupora Mil. 100/- kwenye Godoro.
Malalamiko hayo yalitolewa na Salunge kwa simu alipokuwa akitoka kituo cha Polisii Songe ambako anadai hakupata Ushirikiano kama ilivyokosa kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Juma Abdalahamani, ambapo sasa amehifadhiwa na ambao hawakuvunjiwa.
Akizungumzia tukio la Uvunjaji Salunge alisema, walifika watu watatu Ismail Mwinchande, Kimanzi Msafari na Salum Sokoro toka Korogwe, ambapo alidai wametumwa na Rais Jakaya Kikwete na ndipo walianza kufumua mabati ya nyumba bila kuwapa Notisi na kutoweka na Mil.100/- zilizokuwa kwenye Godoro.
“nilipofanyiwa unyama , niliwaona viongozi wa Serikali ya Kijiji akiwemo Mwenyekiti wa Serikali Abdalahamani nikakosa msaada, Diwani wa Kata ya Kinde Bonge na Polisi Songe nao hawajanisaidia chochote nikarudi na kuhifadhiwa na wasamaria vyombo vikiwa nje”,alisema.Salunge ambaye ni Mkulima.
Mwandishi aliongea na Sokoro na kudai yeye si Msemaji isipokuwa Mkurugenzi Msafiri au Kaimu Mwinchande, na kukanusha yeye na viongozi wake kupora Mil. 100/- akisema hao wanatapatapa kwani walipokwenda kuvunja nyumba hiyo ambayo si ya waliyemkusudia, Sheria zilizingatiwa na walikwenda na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Abdalahmani.
Kaimu Mkurugenzi wa Jupitor Mwinchande alipohojiwa alisema, wao wamepewa kibali na Baraza la Ardhi Korogwe, Madai ya kwamba wametumia Jina la Kikwete kuvunja nyumba hiyo siyo ya kweli, ila mdaiwa Nassoro anawatumia aliowauzia Ardhi ya ndugu yake aliyeko Negero Mvomero kinyemela, ili kuichafua Kampuni, lakini akamtuhumu kutumia Morani wa kimasai kuwatishia maisha.
Aidha Mbunge wa Kilindi Beatrice Shelukindo alipotafutwa kwenye simu ili kuzungumzia Sakata hilo simu yake haikupatikana, lakini Mkuu wa Wilaya hiyo Selemani Livowa alisema yuko kwenye kikao atawasiliana na mwandishi baadaye.
No comments:
Post a Comment