Yaya Toure |
ABU DHABI, Falme za
Kiarabu
MCHEZAJI Bora wa Mwaka 2012 wa
Afrika, Yaya Toure amerejea rasmi mazoezini na kikosi cha timu ya taifa ya
Ivory Coast ‘Elephants' huko Abu Dhabi,
baada ya kukosekana kwa siku mbili kutokana na homa.
Elephant wako huko kujiandaa
na fainali za Mataifa Afrika 2013 zinazotarajia kuanza hapo Januari 19, ambpo
alilazimika kukosa mazoezi kwa siku mbili na kuzua shaka ya kutowweza kuwa
sehemu ya kikosi katika mashindano hayo.
Kaka na nyota mwenzake wa
klabu ya Manchester City ya England, Kolo Toure, ambaye pia yupo na kikosi cha
Ivory Coast, amepata ruhusa maalum kutoka kwa jopo la madaktari, baada ya
kuzuia kufanya mazoezi na wenzake.
"Yaya alikuwa nje ya
mazoezi kwa siku kadhaa," Kolo aliiambia tovuti rasmi ya klabu yao na kuongeza kuwa, kwa
sasa ndugu yake huyo; "Amerejea baada ya kuruhusiwa".
Ivory
Coast inayopewa
nafasi ya kutwaa ubingwa huo nchini Afrika Kusini, imepangwa katika Kundi la
Kifo la D, linalojumuisha mataifa ya Togo,
Algeria na Tunisia.
Katika maandalizi yao ya mwisho kuelekea fainali hizo, Ivory Coast inatarajkia kupimana ubavu na Misri
hapo Januari 14, kabla ya kutua nchini Afrika Kusini – ambako itacheza mechi
yake ya ufunguzi hapo Januari 22 kwa kuwavaa Togo ‘The Hawks’.
No comments:
Post a Comment