HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 04, 2013

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU VYA SHILINGI MILIONI 9 KWA SHULE ZA SEKONDARI KAGERA

 Toka kulia ni Ofisa Mauzo wa Airtel Kagera, Leonard Maige na Meneja Mauzo wa Kampuni ya Airtel wa mikoa ya Kagera na Kigoma, Peter Kimaro katikati wakikabidhi sehemu ya vitabu vya sekondari vya masomo ya sayansi kwa Ofisa Elimu wa shule za sekondari Kagera, Florian Kimolo ikiwa ni msaada uliotolewa na Airtel kwaajili ya shule za sekondari kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo za Kagera, Hafla ya Makabidhioano imefanyima katika shule ya sekondari  kanyeranyere ya wilaya ya Muleba -Kagera.Mwishoni mwa wiki. Airtel imekabidhi Vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 9
Toka kulia ni Afisa Mauzo wa Airtel Kagera bw Leona Maige na Meneja mauzo wa kampuni ya Airtel wa mikoa ya kagera na kigoma bw. Peter Kimaro wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari kanyeranyere ya wilayani muleba mkoani kagera wakiwa wameshikiria vitabu vya sayansi na hisabati walivyokabidhiwa na kampuni ya Airtel mwishoni mwa wiki.Vitabu vilivyokabidhiwa vinathamani ya shilingi
milioni 9


Shule za sekondari za kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo
Kagera zakabithiwa vitabu hivyo
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa shule yetu
imeendelea kutoa mchango wake katika sekta ya elimu ili kuboresha
elimu, kuongeza idadi  na ufaulu wa wanafunzi wa sayansi na kupunguza
uhaba wa vifaa vya kusomea mashuleni.  Airtel imefanya hivyo kwa kutoa
msaada wa vitabu vya kufundishia katika shule 3 za sekondari zilizoko
Mkoani Kagera mwishoni mwa wiki hii.

Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivi ni pamoja na shule za
sekondari za  Kanyeranyere iliyoko muleba, Kirushya wilayani Ngara
pamoja na Nyamigogo iliyoko Biharamuro  kagera

Akiongea wakati wa halfa fupi ya kukabidhi vitabu vya masomo ya
sayansi na hisabati  Afisa elimu wa shule za sekondari mkoani Kagera
Florian Kimolo alisema" shule nyingi za sekondari katika mkoa wa
Kagera zimekuwa na upungufu mkubwa wa vifaa vya kujifunzia na
kufundishia sanjari na uhaba wa vifaa vya maabara na walimu.Kutokana
na upungufu wa vitendea kazi katika shule mbalimbali za sekondari hapa
nchini  tunaomba wadau  wa elimu kujitokeza katika kusaidia kulitatua
tatizo hilo ili shule hizo ziweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Tunashukuru sana Airtel kwa mchango wao katika elimu na katika
kuhakikisha tunapata wanafunzi wengi wa masomo ya sayansi na walimu
wanapata vitabu vya kutosha katika kufundishia masomo haya na mwisho
kupata ufaulu wa kiwango cha juu.

Naye Meneja  mauzo wa Airtel katika mikoa ya Kagera na Kigoma Peter
Kimaro alisema " Airtel imejipanga kuendeleza ushirikiano na serikali
ili kuisaidia wizara ya elimu kufikia malengo waliojiwekea ikiwemo
upatikanaji wa vitabu mashule na kuongeza kiwango cha  ufaulu. Hadi
sasa kwa kupitia mradi wa " shule yetu tumeweza kufikia shule nyingi
za sekondari nchini. Na nimatumaini yetu vitabu tunavyowakabidhi leo
vitaleta mabadiliko ya elimu kwa shule hizi na mkoa wa Kagera kwa
ujumla.

Naye mkuu wa shule ya sekondari Kanyeranyere iliyoko wilyani Muleba
mkoani Kagera alitoa shukurani kwa niaba ya walimu wakuu wa shule za
sekondari za kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo na kusema,
tunashukuru Airtel kwa kuzikumbuka shule za mkoani Kagera, tunaahidi
kuvitumia vizuri vitabu hivi ili kuleta ufanisi zaidi na maendeleo ya
kitaaluma katika shule zetu.

Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia vitabu mashuleni,
zaidi ya shule 900 za sekondari hapa nchini zimenufaika kupitia
kampeni ya mradi wa kampuni ya simu za mkononi Airtel ujulikanao
"Airtel  shule yetu".

No comments:

Post a Comment

Pages