Ofisa Mauzo wa Ecobank, Jakline Nyangoe
(kushoto) akiwafafanulia jambo wageni waliofika katika banda la maonyesho la
benki hiyo wakati wa sherehe ya mwaka wa Kichina iliyofanyika katika viwanja
vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam Februari 3 2013.
Wakazi wa Dar es Salaam na wageni
mbalimbali wakiangalia bidhaa za benki ya Ecobank katika banda la maonyesho la
benki hiyo wakati wa sherehe ya mwaka wa Kichina zilizofanyika katika viwanja
vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam juzi.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akipata taarifa kutoka kwa Balozi wa China Nchini Tanzania
Lu Yuquing wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri
Mkuu ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara,
na Kaimu Mkuu wa Mkoa, Pia Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi. (Picha na Mpigapicha Wetu)
DAR ES SALAAM, Tanzania
Ecobank Tanzania ambayo ni mojawapo ya benki katika kundi la Ecobank Africa iliyo katika nchi 33 Africa, inazidi kukuza uwezo wa wanabiashara Tanzania katika kushiriki biashara kati ya Tanzania na China kwa kupunguza garama za uendeshaji biashara kati ya nchi hizi.
Ecobank Tanzania ambayo ni mojawapo ya benki katika kundi la Ecobank Africa iliyo katika nchi 33 Africa, inazidi kukuza uwezo wa wanabiashara Tanzania katika kushiriki biashara kati ya Tanzania na China kwa kupunguza garama za uendeshaji biashara kati ya nchi hizi.
Wakishiriki katika sherehe ya mwaka mpya ya China Jumapili hii katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Ecobank ilionyesha
nia yake ya kusaidia jamii ya waendesha biashara kati ya Tanzania na
China zikiwepo huduma zinazorahisisha wafanyabiashara
wa Tanzania na wawekezaji
wa Kichina kushiriki katika
uagizaji na mauzo ya nje kati ya nchi hizi.
"Sisi tunayo nia ya kutoa huduma za garama nafuu na
kurahisisha upatikanaji wa bidhaa hizi kuwezesha sekta hii inayokua kwa kasi
sana. katika mwongo uliopita kumekuwa na uwekezaji wa $ 868
bilioni wa china ndani ya Tanzania, huduma zetu zinajaza pengo
la kurahisisha biashara hii "anasema Bw Enoch Osei-Safo,
Mkurugenzi Mtendaji Ecobank Tanzania.
Ecobank inazindua huduma ya kubadilisha
hela ya Tanzania kupata sarafu za kichina (RMB) moja kwa moja, ambapo hapo
awali hapa Tanzania, wanabiashara walilazimika kubadili TZS kwa Dola za
kimarekani ili kununua RMB. Katika mfumo huo wa awali, wanabiashara walipoteza
kiasi kikubwa cha mtaji lakini sasa, Ecobank itatwawezesha wanabiashara
kupunguza garama hizi kwa kueneza huduma hii hapa Tanzania.
" Sisi hatuwezi kupuuza matokeo
ya biashara ya China juu ya Afrika, ambayo inafikia zaidi ya dola bilioni 200 katika mwaka 2012 kwa uagizaji na 5% ya mauzo yote ya Afrika kwenda nchini China,
ushirikishwaji wa kifedha kukuza sekta hii ni muhimu, na
ndiyo maana Ecobank Group imeonyesha
nia ya kurahisisha uendeshaji wa biashara hii na kuwezesha Afrika kuwa na ushindani na nchi zingine duniani.”
Enoch aliongeza.
Ecobank Tanzania katika miezi michache
ijayo itakua kituo cha kutoa huduma za uendeshaji biashara kati ya Tanzania na
China kwa kutoa huduma ya ubadilishaji wa sarafu ya kichina na pia kulipia kodi
ya forodhani kwa TRA papo kwa papo kupitia huduma ya Asybank katika matawi yote
ya Ecobank.
Kwa maelezo zaidi, tembelea: www.ecobank.com
No comments:
Post a Comment