HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 08, 2013

AUWAWA AKIGOMBANIA MWANAMKE MTAA WA ITIJI, MBEYA

Mwili wa marehemu Daniel Mwasalemba, 30, ukiwa umelazwa kwenye majani baada ya kutolewa katika chumba alichouliwa baada ya kuchomwa visu na vitu vyenye ncha kali. Kisa cha ugomvi uliosababisha kifo cha Daniel ni kugombea mwanamke aliyetajwa kwa jina la Elizabeth Michael. (Picha na Kamanga/Mbeya Yetu Blog)
Anayedaiwa kusababisha kifo cha Daniel, ambaye ni muosha magari wa Kampuni ya Sumry jijini Mbeya aliyejulikana kwa jina moja la Peter akiwa na majeraha baada ya kupokea kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.
Hapa Peter akiokolewa na Askari Polisi waliowahi kufika eneo la tukio asubuhi ya leo.
Hiki ndicho chumba kilichofanyikia mauaji ya Daniel katika ugomvi wa kugombea mwanamke.
Baadhi ya ndugu wa marehemu Daniel wakilia kwa uchungu baada ya kuuona mwili wa ndugu yao huyo.
Haikuwa kazi rahisi kwa askari na wanausalama wengine kuzuia hasira za wananchi. Pichani wanausalama hao wakijitahidi kumuokoa Peter asiendelee kupokea kipigo kutoka kwa wananchi hao.
Hapa Peter akiwa amelala chini baada ya kipigo kilaki kutoka kwa wananchi wenye hasira.
Hapa Polisi wakiwa wamepakia garini mwili wa marehemu Daniel aliyeuawa katika ugomvi wa kugombea mwanamke, tayari kwa kuupeleka hospitali kwa uhifadhi, uchunguzi na taratibu nyingine. Mungu ailaze roho ya marehemu Daniel mahali pema PEPONI, Ameen. Bwana alitoa, kisha ametwaa, jina lake lihimidiwe. Inna Lillah Wainna Ilaiyh Rajiuu, Kulun Nafsin Dhaikatul Limauti.

No comments:

Post a Comment

Pages