HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 07, 2013

WANACHAMA WA NSSF KUWASILISHA MICHANGO KWA M-PESA

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori. (kushoto) akibadilishana hati na Mkuu wa Chapa na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa wakati wa kutambulisha mfumo mpya wa kuwasilisha michango ya uanachama wa NSSF kwa njia ya M-Pesa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Kiongozi Mahusiano, Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kulia) akiwa katika mkutano huo.
Wawakilishi wa NSSF.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akifafanua jambo wakati wa kutambulisha mfumo mpya wa kuwasilisha michango ya uanachama wa NSSF kwa njia ya M-Pesa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Chapa na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa.
Baadhi ya Wakuu wa Idara wa NSSF.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akifafanua jambo.
Wadau wakifuatilia.
Baadhi ya wadau waliohudhulia hafla hiyo.
Mkuu wa Chapa na Mawasiliano wa  Vodacom, Kelvin Twissa akifafanua jambo.
Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano, Kelvin Twissa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu utaratibu mpya wa wanachama wa NSSF kuchangia mafao yao kupitia kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori.

DAR ES SALAAM, Tanzania

ZAIDI ya wanachama 6,000 wa Mfuko wa taifa wa hifadhi ya Jamii (NSSF), kuanzia sasa hawana tena sababu ya kutembelea ofisi za mfuko huo kwa ajili ya kuwasilisha michango yao kutokana na kurahisishwa kwa utaratibu wa uwasilishaji michango ambapo kuanzia sasa wanaweza kufanya hivyo kupitia simu ya mkononi kwa njia ya M-pesa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi wa uendeshaji NSSF, Crenscentius Magori alisema utaratibu huo mpya utawaunganisha wanachama wa NSSF na wateja zaidi ya milioni 10 wa Kampuni ya simu ya Vodacom.

“Leo tunatangaza utaratibu mpya na rahisi ambao utawawezesha wanachama wetu hasa walio katika sekta binafs (Informal Sector) kuwa na utaratibu rahisikabisa katika historia ya uwasilishaji michango kwa NSSF kwanjia ya simu ikiwezesha na huduma ya M-pesa” alisema Magori.

Hata hivyo Magori aliongeza kuwa utaratibu huo haufungi utalatibu wa zamani uliokuwa unatumiwa na wanachama wake ambapo alisema vikundi na taasisi kama TUJIJENGE, TAFF, Amsha Group, WANAMA, THT na wanachama wengine kutoka vikundi vilivyojipanga chini ya mfumo wa uwanachama wa hiari vikitazamiwa kunufaika zaidi na mfumo mpya wa M-pesa.

Alisema kupitia uanachama wa hiari katika mfuko huo wa NSSF kila mwanachama huchangia kuanzia sh. 20,000 na kuendelea kwa mwezi.

“Tunataka wanachama wetu hasa waliochini ya mfumo wa uwanachama wa hiari ambao kimsingi hawana mifuko rasmi ya akiba ya uzeeni na hivyo NSSF inmawapatia nafasi ya kujiwekea akiba ili wawe na njia zaidi itakayowapunguzia gharama za uwasilishaji michango yao na hivyo kuendelea kuwekeza kwa siku za baadae” alisema Magori.

Kwaupande wa Mkuu wa chapa ya Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa alisema kasi ya ukuaji wa huduma ya M-pesa nchini inaendelea kuthibitisha uimara na kuaminika kwa huduma hiyo na wadau mbali mbali.

“Kila wakati tunaangalia nikwanamna gani wateja wetu wanavyoweza kuitumia huduma hii kujirahisishia maisha, ahadi yetu kwa watanzania nikuendeleza kuiwezesha huduma hii kuwa salam, yauhakika na kuaminika wakati wote” alisema Twissa.

“Tumesha weza kuzileta takribanbi Nyanja zote za huduma za biashara katika viganja vya wateja wetu kupitia huduma hii ya M-pesa tukiwaunganisha na makampuni zaidi ya 200 kwani kazi ya ubunifu bado inaendelea na wateja wetu watazidi kuona mengi zaidi katika M-pesa ambayo uwezekano wake haukuwarahisi hata kufikirika hapo kabla” alisema.

Alisema huduma ya M-pesa kwa sasa ina mawakala zaidi ya 40,000 nchi nzima na hivyo kuifanya huduma hiyo kuwa karibu na watanzania mijini na vijijini na kuwawezesha kufanya miamala mbali mbali kwa urahisi na uhakika wakati wowote mahali popote ambapo alisema mtumiaji wahuduma ya malipo ya michango hiyo atatakiwa kubonyeza alama ya *150*00# na kuchagua namba 4 ya malipo na kisha kuweka namba ya biashara ikifuatiwa na namba ya uwanachama.

No comments:

Post a Comment

Pages