HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 08, 2013

ENGLAND YAIBANJUA BRAZIL WEMBLEY, YAICHAPA 2-1


 Wachezaji wa England wakishangilia moja ya mabao yao 2-1 waliyoichapa Brazil katika mechi ya kirafiki kwenye dimba la Wembley jijini Londo juzi usiku.
 Wachezaji wa Brazil wakishangilia bao lao wakati wa mechi yao iliyoisha kwa wao kufungwa mabao 2-1 na England katika mechi ya kirafiki iliyopigwa Wembley.
 Fundi: Jack Wilshere wa England (8) akiwatesa mabeki wa Brazil katika mechi hiyo.
 Mtaalamu: Ronaldinho Gaucho wa Brazil, akijaribu bila mafanikio kumtungua mlinda mlango wa England, Joe Hart katika mechi hiyo.
 Jack Wlishere wa England alikuwa mhimili wa England katika idara ya kiungo, alifanya makubwa kama anavyoonekana pichani.
 Kikosi cha kwanza cha England kiliccoumana na kushinda 2-1 dhidi ya Brazil juzi usiku.
 Kikosi cha kwanza cha Brazil, kilichokubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa England wakati wa mechi ya kirafiki Wembley jijini London.
 Wabrazil wakihaha kumzuia Wlishere.
Kiungo Frank Lampard akiruka juu kushangilia bao aliloifungia England, katika mechi hiyo. Nyuma yake ni mfungaji wa bao jingine, Wayne Rooney.
LONDON, England

Huo ni ushindi wa kwanza kwa England dhidi ya Brazil katika kipindi cha miaka 23, na mara ya kwanza kwa kikosi hicho kufunga mara mbili dhidi ya miamba hiyo ya Amerika Kusini tangu mwaka 1984

KOCHA wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson, amekifagilia kikosi chake kwa kupigana kiume na kushinda mechi dhidi ya Brazil katika pambano la kirafiki kuadhimisha miaka 150 tangu kuasisiwa kwa Chama cha Soka (FA.

Mabao ya mshambuliaji Wayne Rooney na kiungo Frank Lampard, yaliipa ushindi England kwenye dimba la Wembley, mbele ya wageni wao na mabingwa mara tano wa dunia, The Selecao.

Akiwa mwenye furaha, Hodgson alisema: “Nimefurahia. Tumethibitisha kuwa sisi ni wazuri vya kutosha. Ni mara yangu ya kwanza kucheza dhidi ya Brazil nikiwa kocha na nina furaha kuona nimekuwa na uwezo wa kusimamia timu kushinda dhidi yao.

“Huu ni ushindi mzuri kwetu. Nina imani hii itawapa wachezaji wangu kujiamini. Jambo muhimu zaidi, lilikuwa kiwango kilichooneshwa na timu.

“Kuna baadhi ya nyakati huwa nzuri sana na sisi tumeonesha thamani ya mabao yetu mawili dhidi ya lao moja.”

Joe Hart kwa namna moja alikuwa nausiku wa aina yake Wembley, alikomudu kuokoa mkwaju wa penati wa mshambuliaji Ronaldinho Gaucho, kabla ya Rooney kuiongoza England kwa bao la dakika ya 27.

Fred akaisawazishia Brazil, lakini Lampard akapigilia la pili na kuizamisha Brazil, kuipa England ushindi uliokuja saa chache baada ya nyota wa Selecao, Neymar kuiponda ‘Three Lions’ kuwa haina uwezo wa kutwaa ubingwa wa Dunia.

Huo ni ushindi wa kwanza kwa England dhidi ya Brazil katika kipindi cha miaka 23, na mara ya kwanza kwa kikosi hicho kufunga mara mbili dhidi ya miamba hiyo ya Amerika Kusini tangu mwaka 1984.

Hodgson aliongeza kuwa: “Wakati unapokuwa kocha wa England na ukawa unacheza kwenye Uwanja wa Wembley unapaswa kujivunia ushindi wowote utakaoipa timu yako.

……The Sun……

No comments:

Post a Comment

Pages