HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 08, 2013

FFU WA NGOMA AFRICA BAND WAPO KAMBINI! KUJIANDAA NA VITA YA 'KUZIBA NYUFA'



 FFU wa Ngoma Africa Band wapo kambini


FFU wa Ngoma Africa Band wapo kambini ! msituni!

Watangaza Vita Mpya ya "KUZIBA NYUFA" katika mpasuko wa Jamii!

Habari za uhakika tena nyeti vimevuja kutoka katika kambi ya bendi
maarufu ya muziki
wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU yenye makazi  yake
nchini Ujerumani.

Kuwa bendi hiyo inayofanananishwa na kikosi kazi FFU imeingia kambini
katika msimu  wa barafu huko ughaibuni,
kwa kujifua na kujiandaa kwa kuwaletea washabiki vitu vipya ! Pia
Kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja
mwanamuziki mwenye mjina mengi ya kutisha tisha kama vile kamanda wa
FFU,Kolokoloni namba 1,mfalme
Hui Hui wa gagagigikoko n.k,kamanda alikaririwa mwanzoni mwa Januari
2013 kuwa Bendi hiyo inaenda kambini
Kujiandaa na vita ! alipoulizwa vita gani? alijibu vita vipya vya
"KUZIBA NYUFA" zilezojitokeza katika jamii yetu!

Ndio kusema Kamanda wetu wa FFU Ras Makunja kaingia kambini na kikosi
chake kujiandaa na vita?
vita venyewe vya kuziba nyufa na mimomonyoko au mipasuko katika jamii
yetu! kauli ya kamanda Ras Makunja
inaonekana inadarubini ya mtazamo mkali unaoona mbali! katika
mahojiano na jarida la africa analysis la Uingereza,

Ni siku chache tu bendi hiyo yenye tabia za ki-FFU ilionekana katika
uwanja wa ndege wa Bremen,wakiwa wanaondoka
lakini wakusema wapi wanako elekea, "wanamuziki wa bendi hiyo wakiwa
na mizigo" nyusoni wakiwa seriously tena  hawakuwa
tayari kujibu chochote wanachoulizwa ! tena katika msimu wa baridi na
barafu wanaenda kambini? tena haijulikani nchi gani?
kama Serbia au Bosnia ? pengine Israel ! hakuna anayejua !

Kamanda Ras Makunja na ffu wa Ngoma Africa Band wapo kambini,kwa
kujiandaa na vita vya kuziba nyufa,
na mwaka huu pia bendi hiyo inatimiza miaka 20 tangu izaliwe mwaka
1993 hadi mwaka huu 2013 ni umri mkubwa.

Washabiki wanasubiri kwa hamu kubwa kuona na kujiunga na na vita
vilivyotangazwa na bendi hiyo chini ya kamanda
Ras Makunja mwenye kichwa kigumu au mkuu wa "Watoto wa Mbwa" Ngoma
Africa ukipenda FFU.

No comments:

Post a Comment

Pages