Na Bryceson Mathias, Mvomero Morogoro
HALI ikiwa si shwari ndani ya Halmashauri ya Wilaya Mvomero Morogoro, Madiwani walitoka nje ya mkutano kususia kikao, huku wakimtelekeza ukumbini Mkurungenzi Sarah Linuma, wakipinga kufaya kazi naye kutokana na kubainika matumizi ya Mil.469,721,961/-bila Uhalili.
Uchunguzi uliofanywa 20.2.2013 nje ya ukumbi wa Halmashauri katika Kikao cha Dharula kilichokuwa kikae kujadili Ukaguzi wa ndani ukiwa na madokezo ya makabrasha, walipoingia na kumkuta Mkurugenzi akiwa amekaa Meza Kuu, waliamua kutoka nje.kuonesha kumkataa.
Madiwani hao wakitarajia kwa barua yenye kumbukumbu MVDC/CPF.49/14 ya tarehe 10.2.2013 waliyomwandikia Mkuu wa Mkoa Joel Bendera yenye kuhusu kukataa kufanya kazi na Mkurugenzi Linuma imeeleweka na kwamba asingekuwepo kwenye kikao hicho walipomuona waliudhiwa na kuamua kutoka nje ya ukumbi wakimteleza na kumsusa hapo hapo.
“Tulishangazwa na Mkuu wa Mkoa Bendera, kuunda Tume ya Uchunguzi wa tuhuma za Ubadhirifu huo badala ya kumchukulia hataua, huku akimuacha Mkurugenzi huyo anaendelea kuwa kazini wakati Mtu akituhumiwa na kuundiwa Tume, hastahili kuwa kazini hadi ukweli uwe wazi.
“Madudu haya ndiyo yanayotumaliza CCM, na hii ni aibu kwa madiwani wake kwa sababu awali zilikuwa tuhuma za malipo hewa ya Ujenzi Mil. 53/-, ubadhirifu wa Mil. 58/-, na sasa Mil. 469,721,961/-, ni aibu kwa Wilaya, Mkoa, Taifa na wananchi. alisema Diwani wao aliyeombwa asitajwe.
Mbali na Taarifa za kwenye Mabrasha, Madiwani tangu kikao cha Dharula cha 28.1.2013 walipinga hayo hali iliyopelekea Watumishi wanne (4), Ester Majagi (Ofisa Mipango), John Kuyi (Mhasibu Matumizi), Anastazia Shosho na Stevin Tibenda (Watunza Fedha). kusimamishwa kazi.
Licha ya Madiwani kumshukia DED Linuma wakidai pengine anahusika na ubadhirifu huo, pia walihoji iwapo kuna ukweli uliozagaa kwamba Mwenyekiti wa Halmashauri Jonas VanZealand ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, kwamba alinunuliwa Magurudumu ya Mil. 6,900,000/-, jambo alilokanusha vikali mbele ya madiwani, hajawahi kupokea hata senti.
Aidha Habari toka ndani ya Halmashauri zimedai kuwepo tuhuma ya Mil.10/- kuchukuliwa ili kufanyia sherehe ya Harusi ya Kigogo mmoja, jambo ambalo linafanyiwa uchunguzi kubaini ukweli wake. Mkuu wa Mkoa Bendera akisubiri taarifa ya Tume yake Madiwani wameipinga na kutishia kuibua Mgorogoro mkubwa wakidai watapeleka mashitaka kwa walipa kodi.
No comments:
Post a Comment