Rebecca Adlington akitangaza kujiuzulu mashindano ya kuogelea mbele ya waandishi wa habari.
Rebecca Adlington akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wake, muda mfupi kabla ya kutangaza kujiuzulu mashindano ya kuogelea mbele ya waandishi wa habari.
Rebecca Adlington katika akiwa na washindi wengine baada ya kujitwalia medali katika mchezo wa kuogelea.
Rebecca Adlington katika akiwa na washindi wengine baada ya kujitwalia medali katika mchezo wa kuogelea.
Rebecca Adlington akipozi akiwa ameshikilia medali ya dhahabu na bendera ya taifa ya Uingereza.
Rebecca Adlington akionesha tuzo ya OBE aliyotunukiwa na Malkia Elizabeth wa II wa Uingereza.
LONDON, England
'Nalichukia sana neno nastaafu. Napenda
sana kuogelea, lakini kufanya hivyo kiushindani kwa sasa sitoendelea, nimefikia
tamati. Daima nitendelea kuogelea hata nikiwa na umri wa miaka 90'
BINGWA
wa medali mbili za dhahabu za michuano ya Olimpiki katika mchezo wa kuogelea, Rebecca
Adlington leo amethibituisha rasmi kustaafu katika katika uogeleaji wa
ushindani.
Majaaliwa
na ya muogeleaji huyo kijana mwenye umri wa miaka 23 katika mchezo huo yalizua
maswali makuu, tangu mkali huyo alipotwaa Shaba mbili za Olimpiki ya majira
ya joto mwaka jana jijini hapa.
Akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari jana jijini hapa, Rebecca mzaliwa wa Mansfield alithibitisha
kuhitimisha zama zake katika mchezo huo, akiwa ametwaa ubingwa wa Olimpiki,
dunia, Ulaya na michuano ya Commonwealth.
'Nalichukia
sana neno
nastaafu. Napenda sana
kuogelea, lakini kufanya hivyo kiushindani kwa sasa sitoendelea, nimefikia
tamati. Daima nitendelea kuogelea hata nikiwa na umri wa miaka 90.'
Rebecca
akaongeza kuwa: 'Kwa hakika siwezi kushinda nao (waogeleaji vijana). Siwezi
kushinda tena katika ngazi hiyo, nahitaji kujiweka mbali kidogo wakati huu hali
yangu ikitengemaa.
'Ilikuwa
muda huo. Beijing
ilibadili maisha yangu yote, kila mmoja alitaka kujifunza kuhusu mimi. Ulikuwa wakati
bora zaidi katika zama zangu mchezoni. Nina furaha sana kuona rekodi yangu ya dunia ingali
imesimama,' alisema Rebecca katika mkutano wake huo.
……The Sun……
No comments:
Post a Comment