Pistorius katikati akifikishwa mahakamani jijini Pretoria, akishtakiwa kwa mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Reeva Steenkamp enzi za uhai wake kabla ya kupigwa risasi na mpenzi wake Pistorius na kufariki dunia Siku ya Wapendao.
Pistorius akiwa katika moja ya mashindano ya mbio za walemavu alizokuwa akishiriki.
JO’BURG, Afrika Kusini
'Polisi inaamini kuwa
siri ya ujauzito aliyopewa ilimfanya Pistorius acharuke na kuingia katika
mabishano yaliyosababisha kifo cha Reeva – kwa kupigwa risasi nne kichwani,
kifuani, mkononi na nyongani'
MWANARIADHA wa mbio za walemavu, Oscar Pistorius anayekabiliwa
na shitaka la kumuua mpenzi wake kwa risasi, amedaiwa kuwa huenda alimuua
mwanamitindo huyo wa zamani akiwa mjamzito.
Kama taarifa hizi
zitathibitishwa, itakuwa mfululizo wa madai unaomuweka nyota huyo kwenye hatari
ya kufungwa kifungo cha maisha – kwa kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp katika
nyumba yake katika usiku wa kuamkia Siku ya Wapendanao.
Katika utetezi wake wa awali, Pistorius alidai kumuua
Steenkamp kwa bahati mbaya, baada ya kuhisi amevamiwa na jambazi aliyejificha
bafuni na kwamba kwa kuwa hakuwa na miguu yake ya bandia, hakuona njia ya
kujihami zaidi ya kufyatua risasi mfululizo.
Ni utetezi uliopingwa na waendesha mashtaka wa kesi hiyo –
waliodai kuwa tukio limefanyika kwa makusudi baada ya mabishano.
Taarifa zilizochapishwa juzi Jumatatu na gazeti la National
Enquirer la hapa zimedai kuwa, huenda mabishano baina ya wawili hao yalitokana
na habari kuwa Pistorius alikuwa akikaribia kuitwa baba wa kichanga cha mrembo
huyo.
Chanzo cha karibu na uchunguzi kililiambia gazeti la udaku
kuwa: 'Polisi inaamini kuwa siri ya ujauzito aliyopewa ilimfanya Pistorius
acharuke na kuingia katika mabishano yaliyosababisha kifo cha Reeva – kwa
kupigwa risasi nne kichwani, kifuani, mkononi na nyongani.'
Chanzo hicho kiliongeza kuwa: 'Baadaye usiku, majirani
walisikia mabishano yaliyofuatiwa na ufyatuaji risasi katika nyumba yao.
'Polisi waliitwa kwa uchunguzi, lakini walijiridhisha tu
kuwa ulikuwa ubishani wa kimapenzi, hivyo hawakuwa na uchunguzi wa maana
waliotarajiwa wangeulizwa kuhusiana na sakata hilo.'
Likiambatanisha na picha iliyopigwa siku chache kabla ya
kifo cha Reeva, gazeti hilo
limeripoti wasiwasi huo, sambamba na habari kuhusu ibada maalum ya kumuombea
marehemu aliyoandaa Pistorius nyumbani kwa mjomba wake anakoishi kwa sasa.
Daily Mail
No comments:
Post a Comment