THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Februari 24, 2013 ameungana na Wakuu
wenzake wa Nchi za Ukanda wa Maziwa
Makuu kutia saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani,
Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mjini
Addis Ababa, Ethiopia.
Mhe.
Rais Kikwete alisema mara baada ya utiwaji saini wa Mpango huo kwamba:
“Hii ni siku kubwa na ya kihistoria kwa watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, jirani zake na Ukanda wote wa Maziwa Makuu. Ni siku ya kukumbukwa kwa
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Afrika, Umoja wa Afrika,
Umoja wa Mataifa na Jumuiya yote ya Kimataifa.
“Watu
wa Kongo wameteseka kwa muda mrefu sana. Wanastahili kupumua sasa. Wanastahili
kuishi maisha bora; maisha ambayo usalama wao umehakikishiwa na kuthibitishwa;
maisha ambayo yatawafanya waendeshe maisha yao kwa kufanya mambo ya maana zaidi
katika kuboresha maisha yao ya kila siku.
“Saini
tulizotia kwa Mpango huo leo ni kielelezo cha dhati na ahadi ya utekelezwaji wa yale yanayotarajiwa na watu wa Kongo na Ukanda
wa Maziwa Makuu kwa ajili ya Amani, Usalama na Ushirikiano.
“Kwa
niaba ya Serikali na Watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naahidi kwamba sisi
tutatekeleza kwa dhati yale yote yanayotarajiwa kwa upande wetu”,
alisema.
Mpango
huo una nia ya kuchangia juhudi ambazo zimefanywa na ICGLR na SADC katika
kutafuta amani Mashariki ya Kongo na ukanda wote wa Maziwa Makuu kwa ujumla.
Mpango
huo pia umetilia maanani mapendekezo muhimu yaliyokubalika baada ya mashauriano
kati ya wakuu wa nchi za ICGLR na SADCna
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Mapendekezo
ya mpango huo ni pamoja na kuboresha sekta ya Ulinzi na usalama, hususan jeshi
la polisi, Kuimarisha mamlaka ya nchi hasa mashariki ya Kongo; na kuendeleza
ajenda kuhusu maelewano, kuvumiliana na kudumisha demokrasia nchini humo.
Vile
vile, nchi za Kanda zimetakiwa kutoingilia mambo ya ndani ya nchi jirani,
kututoa msaada wowote wa vikundi vya waasi, kuheshimu utawala na maeneo ya nchi
jirani na kuimarisha mahusiano ya Kanda.
Hali
kadhalika, Jumuiya ya Kimataifa imetakiwa kuisaidia DRC na Kanda yote ya Maziwa
Makuu kwa ujumla katika utekelezaji wa miradi muhimu pamoja na mkataba wa
Amani, Usalama na Maendeleo katika Ukanda wa Maziwa Makuu.
Aidha,
Mpango huo unapendekeza kuwepo kwa chombo cha usimamizi (Oversight Mechanism)
ambacho kitaundwa na viongozi wote wa nchi 11 pamoja na Umoja wa Mataifa, SADC
na ICGLR.
Imetolewa na:
Muhidin
Issa Michuzi,
Mwandishi
wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Addis Ababa,
ETHIOPIA.
24
Februari, 2013
No comments:
Post a Comment