Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo kuhusu maandalizi ya tamasha hilo. (Picha na Habari Mseto Blog)
DAR ES SALAAM, Tanzania
WARATIBU wa Tamasha la Pasaka,
Kampuni ya Msama Promotions wamesema mikoa iliyoshinda nafasi ya uwenyeji wa tamasha
hilo kwa mwaka huu, imefikia mitatu baada ya Dar es Salaam kuwa wa kwanza
kujitwalia nafasi hiyo kwa wingi wa kura.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Kamati inayohusika na uratibu wa tamasha hilo la kimataifa, Alex Msama, mikoa
iliyoongezeka ni Mbeya na Iringa kwani wapenzi na wadau wa huko wamejitahidi
kutuma maombi
kwa utaratibu ambao waliuweka.
Msama alisema mikoa hiyo mitatu
ndio imepatikana kati ya saba hadi sasa kwa ajili ya tamasha hilo ambalo kwa
mwaka huu litabeba ujumbe wa Amani na Upendo kwa watu wote kwani bila vitu
hivyo, hakina kinachoweza kupangwa na kufanikiwa.
“Tumeamua Tamasha la safari hii
libebe ujumbe huu kwani kuna kila dalili kuwa baadhi yetu tumeanza kuichoka
amani, hivyo tunataka kufikisha ujumbe huu kwa Watanzania kama kuwakumbusha kwa
vile ikipotea, ni vigumu kuirejesha,” alisema.
Alisema wameona ni jambo jema
kwa tamasha hilo kubeba ujumbe huo kwa lenyewe pia limekuwa kielelezo cha amani
na upendo sio tu kupitia ujumbe wa neno la Mungu ambao hupatikana kwenye
nyimbo, pia limekuwa likiwaleta wengi pamoja bila kujali tofauti za dini.
Msama alifafanua kuwa, kwa
jijini Dar es Salaam, tamasha hilo litafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini
Dar es Salaam hapo Machi 31
kabla ya kuhamia Uwanja wa Samora, Iringa hapo April mosi na Uwanja wa Sokoine,
Mbeya.
Naye
Janeth Christopher ambaye ni muimbaji wa injili chipukizi alisema fursa ya
kuwapata waimbaji watakaoshiriki itawasaidia kwa sababu walikuwa hawana namna
ya kuweza kupata nafasi ya kushiriki.
Janeth alisema awali walidhani kwamba, tamasha linaendeshwa kwa
mfumo wa mtu mmoja ambaye ni Alex Msama kumbe linatushirikisha hata sisi wadau,
jambo ambalo anaipongeza kamati ya maandalizi kwa kuwaona.
Aidha wakati taratibu za maandalizi ya tamasha hilo zikiendelea,
wadau wanatakiwa kupiga kura katika mikoa yao ili kukamilisha mikoa
takribani saba ambayo
inategemewa kufikiwa na tamasha hilo, wadau wanatakiwa kupiga kura kwa kuandika
neno gospo halafu jina la mkoa unaotaka lifanyike na utume kupitia namba 15522.
Wakati zoezi hilo likifanyika,
litakalofuata ni zoezi la kuwapata waimbaji washiriki ambao nao watapatikana kwa kuandika
neono gospo, jina la mwimbaji, kikundi au kwaya na kuituma kwendanamba 15678.
Tangu kuasisiwa kwa Tamasha
hilo mwaka 2000 kwa lengo la kueneza neno la Mungu kwa njia ya nyimbo, pia limekuwa
faraja kwa wenye mahitaji maalumu.
No comments:
Post a Comment