HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 08, 2013

Wabunge wakifanya haya, Mwananchi wa kawaida afanye nini?


Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma.

Na Bryceson Mathias

HIVI karibuni Februari 3, 2013 Mbunge wa Tabora Mjini Ismael Aden Rage, kwa mara nyingine alikumbwa na tuhuma ya kusababisha Kujeruhiwa kwa watu watatu eneo la Mwanga Baa Dodoma, ambapo kisingi siku za nyuma zilitundikwa bendera za Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA).

Vurugu hizo zilizotokea kati ya wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wafuasi wachache wa CHADEMAwaliokuwa eneo hilo na baadhi ya wabunge wa CCM, akiwamo Rage, walipokuwa wakigombea Mlingoti wa Bendera ya Chama hicho cha Ushindani bungeni.

Wabunge wa CCM wanaotegemewa ambao siku hiyo heshima zao zilidondokewa na maji taka ya vurugu hizo ukimuacha Rage ni pamoja na Seleman Jafo, Said Mtanda, Nyambari Nyangwine na Mary Chatanda ambaye Arusha anadaiwa kuwa Chanzo cha Mgororo wa Kisiasa.

Kitendo hicho kilipelekea watu watatu kujeruhiwa na wengine kushonwa nyuzi kadhaa kichwani, ambapo wapiga kura na wananchi nchini nikiwemo mimi tunajihoji, ikiwa wabunge tunaowategemea kuwa kioo walifanya hayo, wananchi wa kawaida na walalahoi wafanye nini?.

Ingawa Rage amekana kuhusika na vurugu hizo akisema anaamini uchunguzi kuhusu tukio hilo utamuweka huru baada ya kufikishwa mahakamani kwa sababu hakushiriki wala kumpiga Mwanachama wa Chadema aliyetangaza kumburuza Mahakamani, kipo cha kujifunza.

Adeni; “Sikumpiga mtu huyo!!. Historia yangu inaonesha kuwa sijawahi kushiriki vitendo vya vurugu wala mapigano kwa sababu yoyote ile. 

“Mimi siyo mhuni wa kupiga mtu, nilichofanya ni kumlinda yule kijana asipigwe na wana CCM waliojaa hasira kutokana na yeye kuingilia mkutano wetu,” alisema Rage, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Timu kongwe inayoyoheshimika nchini, Klabu ya Simba.

Pamoja na kwamba Rage na baadhi ya Wabunge wa CCM waliohusika na Vurugu hizo walidai  Kada wa Chadema ndiye aliyekuwa chanzo cha vurugu zilizoishia kwa wana CCM kuwajeruhi makada hao baada ya kuvamia eneo la mkutano wa chama chao, Madai ya Mashuhuda wanasema, 


"Kundi Dogo la wafuasi wa Chadema lililokuwepo eneo la mkutano lilikuwa pembeni kwenye Bendera ya cho bila kufanya vurugu yoyote, ambapo Rage anadai aliwasihi wenzake waachwe wasikilize sera za CCM, kwani mkutano ulikuwa wazi kwa wote bila kujali Itikadi za Vyama".

Viongozi wa Chadema katika maelezo yao walikanusha usemi huo na kusema, Vurugu hizo zilizuka baada ya wafuasi wa Chadema kukasirishwa na kitendo cha vijana wa CCM kung’oa bendera yao wakati wakiendesha mkutano kwenye eneo la Mwanga Baa mjini Dodoma.

Walisema, Wafuasi wa Chadema walilazimika kurudisha bendera yao wakati mkutano ukiendelea, na ndipo makada wa CCM waliojumuika wabunge wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, walipoamua kuwapiga kwa kuwarushia mawe wafuasi hao na kusababisha kuumia kichwani kwa kada watatu wa Chadema.

Ijapokuwa mtu akiugua Vidonda vikapona Makovu hubaki mwilini na kumtia mtu huyo hatiani, ndivyo ilivyojiri kwa Rage, maana pamoja na kukana kuhusika na Vurugu hizo, kulimnyima kuponyoka na Tuhuma hizo, hasa kutokana na kumbukumbu ya matukio yaliyomtokea huko nyuma.

Wakati wa uchaguzi mdogo Igunga 2011, Rage alitozwa faini ya Laki 100,000/- kwa kosa ka kuhutubia Mkutano wa Kampeni akiwa na Silaha (Bastola Kiunoni), jambo lililopelekea Ushindi wa aliyekuwa Mbunge wa Igunga Dk. Dalaly Kamfumu kutenguliwa na Jaji Mary Shangali.

Aidha akiwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa FAT 2005, Rage alituhumiwa kwa upotevu wa Mil. 3,000,000/- za vifaa vya Taasisi hiyo na kuhukumiwa kwenda Jela miaka mitatu, hata hivyo alitoka kwa Msamaha wa Rais kwa wafungwa na kukata rufaa ya kesi iliyomtupa Jela akashinda.

Akiwa Wabunge wa CCM waliohusika na tukio hilo ukiacha Rage ni pamoja na Seleman Jafo, Said Mtanda, Mary Chatanda na Nyambari Nyangwine, na Chatanda, kwa mara nyingine amekumbwa na Adha ua kujeruhi, safari hii akilalamikiwa kuwa chanzo cha sehemu ya Vurugu hiyo.

Sitaki niseme wabunge hao wanapenda vurugu lakini tusemezane ukweli; Kama wabunge walio kioo chetu wanafanya hivyo walivyofanya; Je, wananchi wa kawaida wafanye nini? Kuna vitu vingine kwa wadhifa wako unabidi uviepuke usilitie Taifa aibu na fedheha. Je hayo baadhi ya wabunge wanayajua wajiepushe nayo?.

Kama angefanya mambo hayo mtu wa Chama kingine, mtu wa kawaida Mlalahoi, ambaye Chama chake si Kikuu ingekuwaje? Lawama zangu kubwa juu ya vurugu zilizojiri, nataka sana agharabu nimpelekea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi.

Nampa Lawama hizo nikimtaka asisahau msemo wa Mkuki kwa Nguruwe lakini kwa Bindamu Uchungu!. Ni hivi karibuni kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alizuia Mikutano ya Vyama akidai isifanyike mkoani kwake kwa sababu kuna Vikao vya Bunge.

Amri hiyo ilizuia Mapokezi ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema yasifanyike ambapo Nakala nyingi za zuio hilo zilisambazwa kwenye vyombo vya Ulinzi ikiwamo Polisi. Hiyo si mara ya kwanza lakini hata huko nyuma Chadema waliwahi kufanya Mkutano uliotanguliwa na kibali cha Polisi, lakini baadaye wakashitakiwa.

Ndani ya Wiki moja, Bunge likiwa bado halijaondola Dodoma, Mwenyekiti huyo huyo wa Ulinzi na Usalama anafumbia macho bila kusema lolote na kuruhusu CCM wafanye Mkutano uliozaa Masahaba ya Watu watatu kuumia na kushonwa nyuzi kadhaa vichwani mwao, huku wabunge wa CCM wakishiriki.

Najihoji; Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama ameshindwa kuona uvunjifu wa Amani wakati wa Mikutano ya CCM anauona uvunjifu huo kwa vyama vya upinzani?  Pale Mwanga Baa anayepajua, ni katika ya Mji penye watu wengi kuzidi orodha ya Wabunge na Dk. Nchimbi anafahamu hilo. Je sasa watu wamueleweje watu wamueleweje Dk. Nchimbi? 


Hakuna dhambi mbaya ya Wakristo kama kula Matapishi ya Uongo wa Kauli yako Mwenyewe. Aliyesema Usizini, ndiyo huyo huyo aliyesema Usiue. Siamini kama aliyesema Usiue kama maandiko yanavyosema hakuna mahali aliposema Uzini!! Biblia amabayo hata Dk. Nchimbi anaitumia na saa nyingine kuihubiri kwa Imani yake haisemi hivyo. 

Nataka nithibitishe ukengeufu wanaofanya watu mbele ya Mungu wao kwa maandiko, kuliko kusema bila vielelezo ili tusisutane uongo au kulaumiana bali tuwekane sawa na kuelezana kweli hasa viongozi mnaokaa penye Ukuu ili musiaibike kwa kuwa na kauli mbili.



Kinachoniumiza,  kunishangaza, na wakati mwingine kututia aibu, ni baadhi ya watanzania wenye nyadhifa za heshima, ni kuugeuza ukweli wa Mungu kuwa Uongo. Tunakuwa wazuri wa kubwbwaja, kuandika na kusema, lakini katika utekelezaji kwa uadilifu, tunatisha na kumuudhi Mungu, jambo tunalolisababishia Taifa lipate Mapigo na Laana toka kwa Mungu.

Dk. Nchimbi. Ukiwa na watoto wengi mmoja anaitwa CCM, DP, Chadema, NCCR- Mageuzi, CUF na wengine na wengine... Je, kwa nini kwa huyu  useme Siyo Siyo na kwa yule  useme Ndiyo Ndiyo? Kosa hilo lilimsababishia Aibu Mama yake Esau na Yakobo pale alipotaka akubadilisha uzaliwa wa Kwanza wa Esau auchukue Yakobo mbele ya Mumewe, na hapo ndipo mnapopotoka na kusababisha Vurugu na uvunjifu wa Amani.


Haya endeleeni; Lakini Darubini ni Watu, Vyombo ni Msaada tu!!.



0715-933308

1 comment:

  1. KWA KWELI NI HATARI, KAMA WABUNGE WA CCM WANAFANYA KAMA WALIOVYOFANYA WABUNGE NA VIONGOZI WA CHADEMA KUMDHALILISHA TULE DC WA IGUNGA WAKATI ULE. SASA SIJUI NI KISASI AU CCM NAO WAMEMUA KUWAIGA CHADEMA!!!! SIJUI BWANA.

    ReplyDelete

Pages