HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 01, 2013

BECKHAM AIONYA MAN UNITED KUMCHUNGA RONALDO


PARIS, Ufaransa 

Ronaldo ametoka kuing’oa Barcelona katika Kombe la Mfalme (ikiwa nyumbani Nou Camp) na Beckham analiona hilo kama linaweza kuwa ujumbe tosha kwa Man United – wakati mkali wao huyo wa zamani anaporejea Old Trafford Jumanne

KIUNGO wa zamani wa Manchester United, David Beckham ameionya klabu hiyo kuwa makini na mshambuliaji Cristiano Ronaldo, wakati wa mechi ya marudiano 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa Old Trafford wiki ijayo.

Ronaldo nyota anayechezea klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa sasa, atakuwa ndani ya dimba hilo huku akitazamwa kama mtu hatari anayeweza kumaliza safari ya United katika michuano ya klabu Ulaya msimu.

Hii itakuwa itakuwa safari ya kwanza kwa Ronaldo kurejea ndani ya dimba la Old Trafford, tangu alipoihama Man United mwaka 2009.

Beckham ilimlazimu kusubiri kwa miaka saba kumuwezesha kurejea dimbani hapo kama mchezaji wa tiomu pinzani, wakati alipokuwa akiichezea AC Milan.

Becks, nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England alisema: “Wakati unaporejea, wewe unafurahia tukio, bila shaka, na nina uhakika itakuwa hamasisho pia kwa Cristiano.

“Mambo mengi uhamasisha wachezaji wakubwa na marejeo ya Ronaldo OT itakuwa ni usiku maalum kwake. Mashabiki wanampenda na itakuwa nafasi kubwa na adhimu kwao kumuona tena.”

Man United ilitoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza iliyopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu na Beckham anadai: “United ilifanya vizuri sana ilipocheza Bernabeu na nina uhakika itafanya vizuri sana itakapokuwa Old Trafford.

“Itakuwa mechi kubwa na nzuri kuiangalia. Ni ngumu mno kusema nani atashinda mechi hiyo. Timu mbili kubwa, zinazoundwa na wachezaji wakubwa, hodari na mahiri.”

Becks alienda mbali na kufichua uwezekano wa kubaki Paris Saint-Germain, baada ya kufikia tamati kwa mkataba wa muda mfupi unaoisha kiangazi hiki, ambapo alipoulizwa kama Mei inaweza kuwa mwisho wake San Siro alijibu: “Hakuna lisilowezekana.”

The Sun

No comments:

Post a Comment

Pages