HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 01, 2013

JAPHET KASEBA, MANENO OSWALD WAPIMA UZITO, WATAMBIANA


Mabondia Japhet Kaseba (kushoto) na Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' wakitunishiana misuli wakati wa zoezi la kupima uzito kuelekea pambano lao la kesho Jumamosi kwenye Ukumbi wa DDC Magomeni Kagera.
   Promota wa masumbwi, Pendo Njau akiwa amewashika mikono mabondia Japhet Kaseba na Maneno Oswald 'Mtambo wa Gongo' wakati wa zoezi la kupima uzito lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. 

DAR ES SALAAM, Tanzania

MABONDIA Japhet Kaseba na Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' wanaotarajia kuzichapa kesho kwenye Ukumbi wa DDC Magomeni Kagera, leo mchana wamepima uzito, huku kila mmoja akitamba kumshikisha adabu mpinzani wake hapo kesho. 

Nani kucheka, nani kununa? Jibu litapatikana kesho DDC Magomeni Kagera. Kama we ni mdau na shabiki wa 'ndonga' basi unakaribishwa kushuhudia mtifuano.

No comments:

Post a Comment

Pages