Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu zinazoshiriki michuano ya NSSF Media Cup 2013.
Mwakilishi wa timu ya TBC, Chacha Maginga akipokea jezi pamoja na viatu kutoka kwa Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume. Katikati ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF Juma Kintu.
Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto) akimkabidhi nahodha wa Free Media FC, Salum Mkandemba sehemu ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya NSSF Media Cup 2013 yanayoanza kutimua vumbi Jumamosi Machi 9 kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo kwa wawakilishi wa timu za IPP MEDIA na Mwananchi Communications kwa ajili ya mashindano ya NSSF Media Cup 2013 yanayoanza kutimua vumbi Machi 9 kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM, TANZANIA
MICHUANO
ya NSSF Media Cup 2013 inaanza kutimua vumbi Jumamosi Machi 9, huku ikifunguliwa na Waziri
wa Kazi na Ajira Gaudencia Kabaka, ambapo bingwa wa soka anatarajia kubeba
kombe na pesa taslimu shilingi milioni 4, huku netiboli akitwaa kombe na
milioni 3.
Akizunguza
leo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa, Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume, alisema kuwa, michuano hiyo ya
10 tangu kuanzishwa itashirikisha timu 17 za soka na 15 netiboli.
Michuano
itakayofanyika kwa wiki mbili kwenye viwanja vya TCC na DUCE Chang’ombe,
itafunguliwa leo asubuhi kwa pambano kati ya mabingwa watetezi wa soka Habari
Zanzibar na Changamoto, na Waziri Kabaka atakuwa mgeni wa heshima kwa ajili ya
ufunguzi huo.
Chiume
alizitaka timu shiriki kudumisha amani, upendo na mshikamano wakati wa michuano
hiyo, ili kuipa msisimko na ushindani, ili kujenga taswira nzuri kwa jamii
inayohudumiwa na NSSF pamoja na wanahabari wenyewe ambao ndio wachezaji.
“Sisi
kama NSSF, tunajivunia sifa nzuri tuliyonayo mbele ya jamii, kama ilivyo kwenu
ninyi wanahabari. Tuanatarajia michuano mizuri itakayoondoa tatizo la
udanganyifu, ili kuionesha jamii tulivyo wakweli katika kuwahudumia,”
alisisitiza Chiume.
Alisema
kuwa, gharama ya jumla ya vifaa vya michezo na zawadi ni shilingi milioni 120,
ingawa jumla kuu itakuwa ni shilingi milioni 160, pamoja na zile za matangazo
na huduma kwa wateja (Customer Service), itakayotolewa wakati wa michuano hiyo
kwenye banda maalum.
Mshindi
wa pili wa NSSF Media Cup 2013 kwa upande wa soka atajinyakulia kiasi cha
shilingi milioni 3, huku mshindi wa nafasi hiyo upande wa netiboli ataondoka na
kitita cha shilingi 2. Mshindi wa tatu soka atabeba shilingi milioni 2, huku
netiboli akitwaa shilingi milioni 1.5.
Aidha,
timu ya soka ya Free Media FC (wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na
Sayari), kesho asubuhi inatarajia kufungua dimba la michuano hiyo katika ‘kundi
maalum’ ilikopangwa, kupepetana na Tanzania Standards Newspapers (TSN) kwenye
Uwanja wa TCC.
No comments:
Post a Comment