HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 07, 2013

MAKAMU WA RAIS DK. BILALI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA WADAU WA PSPF LEO

Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal leo amefungua Mkutano wa pili wa Mwaka wa wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) jijini Dar es Salaam na kuzindua uuzwaji wa Nyumba za mradi wa Mfuko huo pamoja na Uchangiaji wa hiyari kwa Watu wasio watumishi wa Umma.

Pichani Meza kuu kutoka kushoto kwenda kulia ni Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Katibu Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini  PSPF, George Yambesi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimkabidhi kitambulisho chake Mwalimu Winfrey Ibrahim Banda baada ya kujiunga na mfuko huo kupitia uchangiaji wa hiyari wakati wa Uzinduzi wake.
Sehemu ya wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea ndani ya Mkutano huo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau (kushoto) akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema wakati viongozi hao wawili walipokutana katika Mkutano Mkuu wa wadau wa PSPF jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa PSPF, Adam Mayingu.

No comments:

Post a Comment

Pages