HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 14, 2013

KINANA ATEMBELEA KIWANDA CHA VIATU CHA TIANJIAN, CHINA


  Katibu Mkuu wa CCM na ujumabe wake wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha viatu cha Huanjian, Dongguan, China baada ya kutembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifunguliwa mlango na Ofisa wa Kichina, ili kuingia kwenye gari tayari kwa safari ya kuondoka jimbo la Dongguan kwenda uwanja wa wa Kimataifa wa Baiyun, Guangzhou kwa ajili ya kwenda jimbo la Chengdu, Machi 13,2013. 
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na ujumbe wake, wakionyweshwa maumbo ya namna kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China. (Picha na Bashir Nkoromo)
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, wakipata maelezo kwa video, kuhusu kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akitazama kiatu, wakati yeye na msafara wake walipotembelea kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China.  Wengine kutoka kwa Kinana ni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Mohamed Yusuf. 
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Titus Kamani (kulia) na Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi, Khamis Suleiman Dadi wakitazama viatu kwenye kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, wakati viongozi hao walipofuatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro wakiwatazama wafanyakazi wa kiwanda hicho.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake  wakiondoka kwenye kiwanda cha Huanjian, baada ya ziara yake kwenye kiwanda hicho.
wafanyakazi wa kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, wakiwajibika na kazi, walipotembelea kiwanda hicho, Machi 13,2013, wakiambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China. 
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, China, akimvisha skafu Ofisa wa Mambo ya Nje wa Jimbo la Dongguan, Sarah Xie, wakati ofisa huyo akiagana na msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Wapili kulia), kwenye hoteli ya Exhibitin Hotel, baada ya Kinana kumaliza ziara yake katika jimbo hilo, Machi 13, 2013 na kwenda jimbo la Chegdu. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhuisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya, Maganga Sengelema na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela na kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi, Khamis Suleiman Dadi. 

NA BASHIR NKOROMO, DOGGUAN, CHINA

WATANZANIA wanaoshi nchini China wametakiwa kukiwa na mshikamano mkubwa na kuitangaza Tanzania kwa kuonyesha tabia njema katika matendo kwa wenyeji wao.

Akizungumza na Wanajumuia ya Watanzania wanaoishi China, baada ya kukutana nao katika mji wa Dongguan, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema, wasipokuwa na mshikamano na kuwaonyesha tabia njema wenyeji wao, Wataharibu sifa ya Tanzania Kimataifa ambayo inafahamika kwamba ni nzuri kwa miaka mingi.

Kinana ambaye hupo nchini China na ujumbe wa watu 14 kwa ajili ya ziara ya mafunzo katika nyanja mbalimbali, alikutana na Watanzania hao, baada ya kuamua kumtembelea katika hoteli ya Exhibition International hoteli, jana, Machi 12, 2013, ili kumsalimia na kubalishana naye mawazo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Watanzania hao walisema,  wamekuwa wakiishi nchini China kwa mahusiano mazuri kutokana na maadili waliyolelewa nayo ya Kitanzania, lakini hali hiyo huenda ikaingia dosari kutokana na kuwepo Watanzania 'feki' ambao wamekuwa wakiingia China kwa pasi za Tanzania na kufanya maovu.

"Hawa Watanazania bandia wakiishaingia hapa hujitambulisha kuwa ni Watanzania, hata wakiulizwa pasipoti ya Tanzania wanayo, lakini cha ajabu ukiwauliza wanakotoka Tanzania wanababaika na hata lugha ya Kiswahili hawajui sawasawa. Utamkuta mtu anajua kusalimia tu, anasema 'mambo' basi, sasa jamani kuna Mtanzania ambaye hawezi kuzungumza kiswahili, lakini akawa na uwezo wa kuja ugenini kama huku?" alisema Katibu wa  Jumuia wa Watanzania hao waishio China, David Chgamla.

Alisema, kutokana na hali hiyo, Wachina sasa wameanza kupunguza imani yao kwa Watanzania kiasi kwamba mtu anapojitambulisha kuwa ni mtanzania wakati akiihitaji huduma anatazamwa mara mbili mbili kuthibitisha uaminifu wake.

Akizungumzia baadhi ya Watanyabiashara kutapeliwa au kuziwa bidhaa zisizo na ubora au kwa bei isiyo halali, Katibu huyo alisema, wengi wanakutana na mikasa hiyo kwa sababu wanakifika China wanakwenda mahali ambapo siyo sahihi kwa mahitaji yao na hivyo kutahamaki wakiingia hasara.

"Lakini Ndugu Kinana, Jumuia hii tuliyounda hivi karibuni na kuwa na uongozi huu mpya, nina imani itawasaaidia Watanzania wengi kutopoteza fedha au mali zao wanapokuwa wamekuja hapa kibiashara, kwa sababu tunajipanga vema kuhakikisha kila atakayekuwa anakuja  akipenda anakutana na sisi kwa ajili ya msaada", alisema.

Uongozi wa Wanajumuia hiyo ya Watanzania unaundwa na John Luhumbiza (Mwenyekiti), Abraham Merishani (Makamu Mwenyekiti),  David Chamla (Katibu Mkuu) na Msaidizi wake ni Aboubakari Mwinyi.


No comments:

Post a Comment

Pages