Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akipa mpira wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Habari Mseto Blog)
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya NSSF leo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akikagua timu ya Changamoto kabla ya pambano lao na timu ya Habari Zanzibar. Changamoto iliwavua ubingwa wa michuano hiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya Habari Zanzibar kwa kuitandika 3-0.
Waamuzi wa mchezo wa ufunguzi wakisalimiana na mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka kabla ya mchezo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisalimiana na wachezaji wa Habari Zanzibar.
Golikipa wa Habari Zanzibar akipatiwa matibabu baada ya kuumia.
Kocha wa timu ya Changamoto, Mawazo Lusonza akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (katikati) akifuatilia mchezo wa netiboli kati ya NSSF na Mlimani Tv, katika mchezo huo NSSF ilishinda 46-1 Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.
Meneja Uhusiano, Kiongozi Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume (kulia) akiwa na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu wakati wa ufunguzi wa mashindano ya NSSF Media Cup leo.
Beki wa timu ya Changamoto, Emmanuel Balele akiruka juu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa wa ufunguzi wa mashindano ya NSSF Media Cup dhidi ya NSSF uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Changamoto imeshinda 3-0
Mshambuliaji wa timya Habari Zanzibar, Amour Mohamed akimtoka beki wa Changamoto, John Robert
Kiungo wa timu ya Changamoto, Andrew Faustin akitafuta mbinu za kumtoka mshambuliaji wa Habari Zanzibar, Thani Mfamau.
Beki wa timu ya Changamoto, Emmanuel Balele akiruka juu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake.
Timu za Nertiboli za NSSF na Mlimani Tv zikichuana ambapo NSSF imeshinda 46-1
No comments:
Post a Comment