HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 09, 2013

TANZANIA YANG’ARA NA VIVUTIO VYAKE VITATU MAONYESHO YA (ITB) BERLIN UJERUMANI

1Wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakigonganisha glasi za mvinyo wa matunda ya Mananasi uliotengenezwa nchini Burundi wakati wa hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)kwenye maonyesho ya utalii ya (ITB) yanayofanyika kwenye jengo la Mense Berlin jijini Berlin Ujerumani, Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa na mkakati wa Kutangaza utalii wa Afrika Mashariki na mwaka huu ilikuwa na kazi moja ya kunadi maajabu manne ya Afrika yaliyopatikana katika ukanda huu wa nchi za Afrika Mashariki ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mto Nile, Mbuga ya wanyama ya Serengeti na Ngorongoro Crater huku Tanzania ikiwa kinara kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa maajabu yake matatu ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya Serengeti na Ngorongoro Crater jambo lililofanya itamkwe mara nyingi miongoni mwa viongozi waliopata nafasi kuzungumzia utalii wa Afrika Mashariki PICHA NA FULLSHANGWEBLOG 2Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akipokea tuzo maalum iliyotolewa na iliyotolewa kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kwa Bi Maria Mutagamba Waziri wa Utalii wa Uganda katika hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye maonyesho ya (ITB) Berlin jana, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa (EAC) Jesica Eriyo 4Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Meena kulia akiwa na Adolf Mchemwa Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania Ujerumani wakiwa katika hafla hiyo 5Bi. Maria Mutagamba Waziri wa Utalii wa Uganda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo akisoma hotuba yake na kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu utalii wa nchi za Afrika Mashariki 6Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Bi Jesica Eriyo akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo ili azungumze na washiriki wa maonyesho hayo pamoja na wageni waalikwa katika hafla hiyo. 7Ken Nyauncho Osinde Balozi wa Kenya nchini Ujerumani akizungmza na wageni waalikwa na kueleza ushirikiano wa Mabalozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Ujerumani katika kutangaza utalii wa ukanda huo 8Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka Tanzania Bi Maimuna Tarishi akitambulishwa rasmi katika hafla hiyo 9Maofisa kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kulia ni Bw. MashauriBrenda Mugambi na Aileen Mallya wakiwa katika hafla hiyo. 10Baadhi ya wageni kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa zinazojihusisha na masuala ya utalii wakiwa katika hafla hiyo. 12Dk. Nyamajeje Wigoro kutoka EAC akisalimiana na viongozi wawakilishi wa nchi za Jumaiya ya Afrika Mashariki kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa (EAC) Bi. Jesica Eriyo. 13Wageni mbalimbali ambao pia ni washiriki wa maonyesho hayo ya utalii kutoka Uganda wakiwa katika hafla hiyo. 15Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Chrisopher Mvula kushoto akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki katika hafla hiyo. 16Dk Nyamajeje Wegoro akishauriana jambo na Rica Rwigamba Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Rwanda katikati ni Bw. Mashauri kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki 17Makatibu wakuu na Mawaziri wa nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi na maofisa wa Utalii wa Nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki 18Makatibu wakuu na Mawaziri wa nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi na maofisa wa Utalii wa Nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki 20Kikundi cha ngoma kutoka nchini Uganda kikitumbuiza katika hafla hiyo. 24Kikundi cha ngoma kutoka Burundi kikitumbuiza katika hafla hiyo 25Wa kwanza ni Waziri wa Maliasili Uganda B. Maria Mutagamba, Balozi wa Kenya nchini Ujerumani Ken Nyauncho Osinde na Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania Bi Maimuna Taarishi wakishiriki kucheza ngoma ya Asili ya Uganda wakati wa hafla hiyo. 26Kaimu 
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula kulia akishiriki kucheza ngoma muziki na wageni waalikwa mbalimbali katika hafla hiyo

No comments:

Post a Comment

Pages