Na Francis Dande
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha
la Pasaka Machi 31 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam .
Kwa mujibu wa taarifa kwa
vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo , Alex
Msama tayari Ofisi ya Waziri Mkuu imeshathibitisha kuhusiana na ujio wake
kwenye tamasha hilo .
“Tunafurahi kwamba tamasha
letu mwaka huu Dar es Salaam
mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mwaka jana alikuwa Waziri wa
Mambo
ya Nje, Benard Membe,”
ilisema taarifa hiyo ya Msama.
Waimbaji mbalimbali wa ndani
na nje ya Tanzania
wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo ,
ambapo wan je ya nchi ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya ,
pamoja na kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali
Rwanda .
Kwa upande wa wasanii wa hapa
nchini watakaotumbuiza ni Upendo Kilahiro,
Rose Muhando, Upendo Nkone na John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na
kundi la Glorious Celebration.
Tamasha la Pasaka litafanyika
Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea
Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora
Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja
wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mbali ya tamasha hilo kuwa na malengo ya
kueneza ujumbe wa neno la Mungu kupitia uimbaji, pia sehemu ya fedha amnbazo
hutokana na viingilio hutumika kuwafariji walemavu, yatima na wajane.
Hata hivyo, kwa mwaka huu
litatumika kufikisha ujumbe wa kusisitiza suala la amani na upendo kwa watu
wote bila kujali dini, itikadi, jinsia wala rangi kwani wote ni wamoja mbele za
Mwenyezi Mungu.
No comments:
Post a Comment