NA DENIS MLOWE IRINGA
MATOKEO ya kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi yamewekwa wazi na msimamizi wa uchaguzi huo, Sule Masanguti, na kuonyesha kuwa mgombea Fredy Fabian Ngajiro ameongoza kwa kupata kura 2,703. Ngajiro, anayefahamika zaidi kama Vunjabei, ameshika nafasi ya kwanza katika mchakato uliovutia wagombea 18.
Akifuatia nyuma yake na Festo Shemu Kiswaga aliyepata kura 868, wakati Emmanuela Kaganda Mtatifikolo ameibuka na kura 682. Arif Abri amepata kura 233.
Kwa mujibu wa Masanguti, wagombea wote 18 waliochukua fomu walirudisha, na matokeo mengine ni pamoja na Dkt. Abdalah Lusasi (100), Claudia Francis (69), Asakwe Widambe (58), Elias Kazikuboma (52), Eng. Sebastian Kiyoyo (37), Josephat Masambwa (34), David Komba (27), Tedson Ngwale (24), Egidy Mkolwe (23), Watende Kiyagi (16), Dkt. Tumain Msowoya (15), Lazaro Francis Gwira (10), Thitho Cholobi (9) na Thobias Mwilapwa (5). Masanguti alibainisha kuwa matokeo hayo ni ya awali huku vikao vya chama vikiendelea kufanya uchambuzi wa kina kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.
Mchuano huo umeonyesha ushindani mkali, lakini Vunjabei ameibuka na nguvu kubwa ya kisiasa baada ya kuongoza katika kata nyingi, ikiwemo maeneo ambayo baadhi ya wapinzani wake wanatoka. Hali hii inaashiria mwelekeo mpya wa kisiasa ndani ya jimbo la Ismani kuelekea kumpata mgombea wa mwisho wa chama katika uchaguzi mdogo ujao.
Baadhi ya wagombea waliotia nia, akiwemo Tumain Msowoya, Lazaro Francis na Arif Abri, wamepongeza mchakato huo wakisema kuwa umeendeshwa kwa uwazi, na kueleza utayari wao kuungana na atakayeteuliwa na chama.
Kura za maoni hizi zimefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Wiliam Vangimbe Lukuvi. Wakati wa kura za maoni za mwaka 2025, Lukuvi aliibuka na kura 5,746, akifuatiwa na Festo Kiswaga aliyepata 1,159. Hali ya sasa inaonyesha kwamba Vunjabei amekaribia kiwango cha kukubalika alichokuwa nacho Lukuvi kwa kupata kura
Wakizungumza na mwanahabari baadhi ya wananchi wamesema kuwa CCM wajue kuwa chaguo la wajumbe ndio chaguo la wananchi mtindo wa kuwabadilisha kwa sababu ambazo wananchi hawajui huleta changamoto katika chaguzi na kukipa wakati mgumu.
Kwa sasa tumempa Fred sasa tunahitaji kijana kama huyu aweze kuendeleza pale alipoishia Lukuvi walisema



.jpeg)


No comments:
Post a Comment