Baadhi ya waendesha pikipiki wakionekana kuwa na hamasa kubwa wakati wakisindikiza msafara wa Kinana kuingia mjini Morogoro leo, (Picha zote na Bashir Nkoromo)
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili eneo la Nane Nane mkoani Morogoro kuanza ziara ya siku nane ya kikazi mkoani humo, leo Aprili 14, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Innocent Edward, wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika eneo la Nane Nane, nje kidogo ya mji wa Morogoro, leo. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro mjini Fikiri Juma. Kinana amewasili mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya siku nane kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa ilani ya CCM.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akijaribu moja ya pikipiki, kabla ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuondoka eneo la Nane Nane kwenda Morogoro mjini kuanza ziara ya kikazi mkoani humo Aprili 14, 2013.
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ukionzwa na waendesha pikipiki baada ya kuwasili mjini Morogoro leo Aprili 14, 2013, Kinana anaaza leo ziara ya kikazi mkoani humo.
No comments:
Post a Comment