Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma
Kikwete, akikabidhi zawadi ya kompyuta mpakato kwa mmoja wa wanafunzi waliopata
daraja la kwanza katika matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2012 wakati wa
sherehe za kuadhimisha mika 10 ya Fao la Elimu la Mfuko wa Pensheni jijini Dar
es Salaam, mwishoni mwa wiki. Katikati
anayeshuhudia ni Mweyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Adolf Mkenda. (Picha na Habari Mseto Blog)
Na Mwandishi Wetu
MKE wa Rais Salma Kikwete ameomba
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi (PPF)
kupitia Fao la Elimu kuwasomesha
watoto mpaka kidato cha sita ili kuweza kuwafanya watoto hao wasikatishe masomo
kutokana na kukosa karo .
Salma aliyasema jana wakati
wa maadhimisho ya miaka 10 Fao la Elimu linalotolewa na Mfuko wa Pensheni kwa
watumishi (PPF),alisema kuwa fao hilo kuwasomesha mpaka kidato cha nne kuna
uwezekano wa kukosa kuendelea na kidato cha tano na sita kutokana kukosa karo
kwa walenzi inayosababishwa na kipato kuwa chini.
Alisema kuwa juhudi ambazo
zimeonyeshwa na PPF kupitia fao la elimu kwa kuwasomesha watoto waliofiwa na
wazazi ambao ni wanachama kumesaidia kuokoa ndoa kwa wasichana wadogo ambapo
wasingeweza kuendelea na elimu kutokana na familia kuwa na kipato kidogo au
kukosa kutambua fursa ya elimu kwa mtoto wa kike.
Salma alisema kuwa ni muhimu
kwa mifungo mingine ya hifadhi ya Jamii kuanzisha utaratibu wa fao la elimu
watakuwa wamesaidia sana katika kusuka gurudumu la elimu kwa watoto ambao
wanaweza kuondokewa na wazazi wakiwa umri wao haujafikia kujitegemea.
Aliongeza kuwa kusomesha
watoto 1333 katika utaratibu wa fao hilo wamesaidia kuweza kuleta chachu ya
elimu kwa familia hizo na kusinge kuwepo kwa utaratibu huo wengine wasingeweza
kusoma jamii inayochiwa kuona suala la
kusomesha watoto ambao wamefiwa na wazazi wao sio jukumu la lao.
Salma Kikwete aliwataka
watoto wanaosomeshwa kupitia fao hilo kujituma na kuja kuwa nguvu kazi ya taifa
yenye tija ya kuzalisha kupitia elimu ambayo wameipata kutokana na mwanga ulionyeshwa
na PPF.
Mwenyekiti wa Bodi wa PPF
Profesa Adolfu Mkenda alisema changamoto kubwa katika fao la elimu ni baadhi ya
watu kupeleka watoto wao na kuachwa watoto waliofiwa na wazazi ambao ni
wanachama wa mfuko huo.
Alisema kuwa watu ambao wanakuwa
wamepewa jukumu la kusimamia familia ya marehemu ambaye ni mwanachama wa PPF
ambapo wanatumia fursa ya kupeleka watoto wao na kuwaacha wahusika wa kupata
haki hiyo.
mwisho
No comments:
Post a Comment