HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 02, 2013

Tusikubali kuvishwa Ufisadi


Na Bryceson Mathias, Morogoro

KWA Imani Musa alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao; akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo (Ebr. 11:24,25).

Kwa ukomavu wa kisiasa, maadili ya dini na Elimu ya Demokrasia waliyonayo watanzania, sasa wanaelewa mema na mabaya kwa hiyo naamini hawawezi Kudhulumu na Kumyima Haki mtu yeyote.

Kama Musa alivyomkimbia Farao, ukiwemo utajiri, elimu aliyoipata na kwenda kuunganika na Wana wa Israeli waliokuwa Utumwani Misri wakati huo na kuwa adui wa   Farao, Hata leo watanzania tunaweza kuikataa Rushwa, Ufisadi na Dhuluma vinavyoitesa nchi yetu.

Musa akiwa mdogo hakujua haki na malezi yaliyoasisiwa na Farao kupitia kwa mwanae  mfalme aliyemuokota Musa akielea kwenye Kitundu Mtoni. Aliona kama amepata bahati ya kuokota mtoto ambaye nyumbani mwa baba yake alikuwa kama Lulu ya Urithi.

Musa ni Mtu kama sisi aliyepata elimu na ufundi wa kila namna Kasri la Farao, ingawa alipata kila kitu, akaishi kwa raha kama mrithi wa Farao, alipopata akili, Hekima na ufahamu Mfalme si Baba yake, na Binti Farao si mama yake alitoa maamuzi magumu.

Watanzania leo tukipata akili ya kwamba, Ijapo Rushwa, Ufisadi na Dhuluma vinawaneemesha baadhi yetu; kwa kuwa tuna akili mpya kama Musa, tunaweza kukakataa na kusema yatosha, kwaheri.

Hata kama UfisadiRushwa na Dhuluma hiyo anafanya Mwekezaji au Mwenzetu, Musa alipopata Uelewa alidai Haki yake na ya wana wa Israeli maana hatustahili kuitwa watumwa wa Farao.

Watanzania tunaweza kuepuka Utumwa wa Rushwa, Ufisadi na Dhuluma na kuamua kuachana navyo kwa kuwa hata sisi hatustahili kuwa watumwa wa watu wachache wanaofanya UfisadiRushwa na Dhuluma kwa faida ya familia zao.

Utajiri, Enzi, na Fahari visitufanye tuuzwe na Watawala wetu kwa aibu ya Ufisadi, Rushwa na kuwa watumwa kwa kukipigiwa Kengele na Filimbi za Rushwa, Ufisadi na Dhuluma masikioni.

 Ni wakati muafaka tukatae ili Laana hiyo isivikamate vizazi vyetu hadi viende kaburini vikiwa na dhambi hiyo.

Inatafsirika alichofanya Musa ni uamuzi wa kijinga, kipumbavu na wa kibinafsi, na wenye kutaka kupandikiza chuki kati yake na watawala! Lakini kimsingi aliepuka Matusi ya kufanywa Mtumwa na Karai la Zege.

Hayo ndiyo mambo mabovu yalimuimiza Musa; Je, watawala wetu, wanasiasa, na viongozi mbalimbali wanaotuwakilisha wakiwemo wabunge mnasutwa na nini juu ya watanzania? Au mnaishia Usingizi na kuhasimiana badala ya kuwatoa watanzania Misri?

Ikifika hapo ndipo ninapoujiliza Swali; kwa  nini Mungu aliuweka mti wa ujuzi wa mema na mabaya katika bustani ya Edeni ilihali akijua utamgharimu, Adamu na Hawa bustanini nyakati hizo?.

Mungu aliuweka mti wa ujuzi wa Mema na Mabaya, ili awape Adamu na Hawa chaguo la kumtii au kutomtii Mungu. Adamu na Hawa walikchagua Laana ya kuwa uchi na kuvaa majani. Wabunge msitufikishe huko!

Maziwa hayaungwi pilipili; mbonaa wabunge mnaruhusu wawekezaji na watu wasio na uchungu wan nchi hii wakiungana na Farao wa Musa, kuunga pilipili kwenye maziwa ya watanzania?

Nina uhakika; Mnaposhindwa na kufanya Uzembe wa kutosema kweli ya kutetea Haki, Rasilimali, Utu, Uhai na Maisha ya Mtanzania, Damu yao inayomwagika kwa dhuluma bila Hatia, itadaiwa mikononi mwenu!


0715-933308

No comments:

Post a Comment

Pages