HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 30, 2025

Kongamano la Madereva boda baoda bajaji na Mama lishe kufanyikaa January 2026

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


Shirikisho la madereva boda boda na bajaji na Mama lishe  wameiomba Serikali kulitazama kundi  hilo kwa kulipatia fursa Mbalimbali ikiwemo mikopo na kuwatengea Mazingira Rafiki


  Akimezungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Desemba 27,2025 Mwenyekiti wa shirikisho Saidy Kagomba amesema January wanataraji kufanya kongamano kubwa la kitaifa linalotarajiwa kufanyika mwezi Januari, 2026 ambapo watawasilisha kero zao zote Serikalini ili zitatuliwe.


 " Kongamano hili halitawahusisha wao pekee, bali litawakutanisha pia viongozi wakuu wa serikali, ambapo  wanatumia fursa hiyo kuwasilisha changamoto zinazowakabili wamachinga, boda boda na bajaji nchini nzima" amesema Kagomba




“Boda boda wengi tunakosa mikopo kwa wakati hivyo tunaomba taasisi za kifedha na serikali kutufikia ili tuweze kujikwamua kiuchumi,” alisisitiza.


Hata hivyo  Mwenyekiti amewashukuru wamachinga na mama lishe kwa kuonesha uzalendo na nidhamu kwa kutoshiriki maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika tarehe 9 na 25 Desemba.


“Nawashukuru sana wamachinga na mama lishe kwa kutii wito wa amani na kutoshiriki maandamano katika tarehe hizo. Hatua hii imeonesha mshikamano na upendo wa nchi,” alisema.


Aliongeza kuwa maandalizi ya kongamano la kitaifa yanaendelea vizuri, huku akisisitiza kuwa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wadogo na waendesha vyombo vya usafiri zinahitaji ufumbuzi wa haraka katika maeneo yote ya nchi.


Akizungumzia changamoto hizo, Mwenyekiti huyo alisema kuwa changamoto ya kwanza kwa waendesha boda boda ni kukosa mikopo kwa wakati, hali inayokwamisha juhudi zao za kujiendeleza kiuchumi.


Aidha, alieleza kuwa waendesha boda boda hukaa muda mrefu juani wakisubiri wateja, hivyo akaomba serikali itengeneze miundombinu rafiki kama maeneo ya kupumzikia na kujisitiri wakati wa kusubiri huduma.


Changamoto ya pili aliyoitaja ni fursa za kifedha, ambapo alieleza kuwa tayari Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameidhinisha zaidi ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya mikopo kwa vijana, wanawake na makundi maalum, huku akiomba fedha hizo ziwafikie walengwa kwa wakati na kwa uwazi.


Pia aligusia changamoto ya mgambo wanaodaiwa kuwasumbua wamachinga katika maeneo mbalimbali, akiiomba serikali kuwatafutia ajira rasmi ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima mitaani.


“Mgambo nao ni Watanzania wenzetu. Tunaomba watafutiwe kazi mbadala ili kuondoa migogoro na kuwapa wananchi mazingira ya kufanya kazi kwa amani,” alisema.


Kongamano hilo linatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kitaifa litakalowakutanisha wadau mbalimbali, likiwa na lengo la kusikiliza, kujadili na kutatua changamoto zinazowakabili wamachinga, boda boda na bajaji nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages