HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 13, 2013

JUMUIYA YA UPENDO KKKT CHINAGALI YAFANYA MAKUBWA


Mchungaji Mama Kobwe akiweka Wakfu Vifaa vya Jumuia ya Upemdo KKKT Chinangali, walivyonunua kutumia kwenye Ibada za nyumba kwa nyumba
Na Bryceson Mathias. Dodoma
IBADA za Jumuia zinazomasishwa  na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dodoma kwenye Sharika na Mitaa, zimeipa MafanikioMakubwa Jumuia ya Upendo ya Usharika wa Arusha Road,ambapo imefikia mahali pa kukuza  mahusiano yao na Makanisa mengine likiwepo Kanisa la Romani Katoliki (RC).
Mafanikio hayo yalibainika katika Ibada ya kuweka Wakfu Vyombo vya Ibada za Nyumba kwa Nyumba zinazofanyika kila siku na Jumamosi saa 12.30 hadi saa 1.30,  iliyofanyika 11.4.2013 vyenya Gharama ya Milioni 1,344,000/- zilizotolewa na waumini hao.
Wakisoma Risala kwa Kaimu Kiongozi wa Jimbo la Makao Makuu (KKKT Dodoma) Mchungaji Alice Kobwe, wana jumuia walisema, jumuia yaotangu ianzishwe na Mlezi wao Amani Osma (Mkulima), imekuwa na Mafanikio Makubwa ambapo sasa ina Mahema ya kufanyia Ibada za Nyumba kwa Nyumba,Viti, Vitambaa, Msalaba na Vitabu vya Ibada hizo.
“Mbali ya kuwa na wanajumuia zaidi ya 108, pia tuna Sadaka Maalum ya kuwatunza wasiojiweza na Wajane, jambo ambalolimetupatia Baraka katika familia, biashara, na kazi zetu za mikono, kutoka na kuwakunjulia watu wenye njaa, kuwashibisha wasiojiweza nafsi zao kama Isaya 58:10 isemavyo.alisema Kaimu Mwenyekiti Doris Mgidange.
Vifaa walivyonunua bei zake kwenye mabano ni pamoja na Viti vya Plastiki 50 (750,000/-), Meza moja (80,000/-), Msalaba (12,000/-), Kitambaa cha Meza ya Ibada, Hema la kukutania (480,000/-) Jumla Milioni 1,344,000/-, ambavyo huhamishwa kwenda nyumba itakakofanyika Ibada siku inayofuata.
Jumuia hiyo ambayo kwa sasa Kauli Mbiu yao ni ‘Mavazi Mazuri kwenye Ibada za Jumapili Uzingatiwe’, pia wamemuomba Mchungaji Kiongozi Kobwe uzingatiwe, na kwamba Mtaa waoni Mkubwa hivyo wanaomba Wazee wa Kanisa wawili,  na kuwatembelea, ambapo aliahidi kufikisha Ngazi za Juu.
Akijibu sehemu ya Hoja, Mchungaji Kobwe alisema, “Kanisa limeweka Mkakati wa Kununua nguo (Kanga) ili kwa mwanamke atakayekwenda kanisani na nguo isiyofaa, kama hatarudishwa nyumbani atavishwa nguo hiyo na kuingia kanisani ahudhurie Ibada”.alisema Kobwe.
Aidha Ibada hiyo ilizihusisha Jumuia za Kanisa la RC za Mtakatifu Agustino  iliyoongozwa na Sospeter Msendekwa na Consolata Remy, zingine za Maili Mbili iliyoongozwa na Godfrey Swai, na Jumuia ya Usomalini ya KKKT iliyoongozwa na Gadi Mahau –Mlezi wa Jumuia, na Magdalena Hezroni.

No comments:

Post a Comment

Pages