Askofu Dk. Jacob Erasto Chimeledya (56) akisimikwa kuwa askofu wa Kanisa la Anglikani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,
akimpongeza Askofu Mpya wa Kanisa la Anglikani Askofu
Dk. Jacob
Erasto Chimeledya (56)
Na Bryceson Mathias
PAMOJA na Rais Jakaya Kikwete kufunguka na kuanza kukemea wanaoendeleza Udini, bado mzimu wa Udini unaendelea kuiandama na kuitesa Serikali yake ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Ingawa akiwa Dodoma wakati wa Sherehe za Kumtawaza Askofu Mpya wa Kanisa la Anglikana la Roho Mtakatifu Dk. Jacob Erasto Chimeledya, bado vitendo vya Uharibifu na Uchomaji wa Makanisa vilikuwa vinaendelea kwa kasi nchini.
Ijapokuwa katika Utawazo wa Askofu Askofu Dk. Chimeledya, Kikwete aliwakemea wanaoasisi na kuhubiri Udini kuwa ni Mashetani, na kwamba Serikali yake haiyawavumilia itahakikisha inapambana nao; vitendo hivyo vilifanyika Tanga.
Kama watu wasiotaka kusikia Kauli ya Rais Kikwete, Maharamia wa Udini huo, jana hiyohiyo walichoma Jengo la Shule ya Watoto ya Kanisa la Kiroho la Betham lililoko eneo la Donge Tanga, Nyumba ya Kituo , na kuchoma Jengo la Kanisa (TAG).
Ilifahamika kwamba 8.usiku katika kanisa la Betham lililoko eneo la Donge wahusika waliteketeza kwa moto jengo la kanisa lililokuwa likitumika zamani na kisha kuingia ndani ya kanisa kubwa la sasa na kuviwasha kwa moto moto vitambaa vilivyokuwa vimefunika Madhabahu.
Usiku huo huo majira ya saa 9 usiku, Tukio jingine la aina hiyo liliripotiwa likihuhusisha kuchomwa kwa Kanisa la Miracle Revival lililopo Makorora ambapo mashuhuda walidai, wakiwa usingizini, walishutuka kuona moto ukiwaka kwenye nguzo za kanisa, ndipo wakapiga kelele za kuomba msaada.
Licha ya Rais Kikwete kuchukizwa na vurugu za kidini zinazoendelea fanywa na baadhi ya watu wasioitakia mema Tanzania, huku akidai watu hao wanajua kuwa Amani ikitoweka nchini ni gharama kubwa kuipata. Ni wakati muafaka kwake kuchukua hatua Kali na ya Wazi kwa wanaohusika anaowasema, ili liwe fundisho wasithubutu tena.
Nadhani Rais sasa asifike kusema tu kama alivyosema Dodoma kwamba, “Wapo watu ambao yakitokea machafuko hapa nchini wao hawaoni tatizo, mfano James Mbatia yeye atakimbilia Kenya, Profesa Anna Tibaijuka yeye atakimbilia Uganda. Lakini wale ambao hawana pa kukimbilia mnafikiria watakimbilia wapi?
Mfano huo ambao aliutolea kwa wananchi wanaotoka mikoa inayopakana na mataifa jirani akisema kuwa vurugu zikitokea wao watakimbilia huko wakati wale wasio na uwezo huo wakitaabika, bado hauwafanyi waharifu hawa kuogoa na ndiyo maana wakati akikemea vitendo hivyo Dodoma, wao wamechoma Makanisa Tanga siku hiyo hiyo.
Binafsi ninajisikia vibaya sana, kama Rais ameweza kukemea tabia hiyo asubuhi kwenye Ibada ya Askofu Dk. Chimeledya iliyohudhuriwa na Askofu Mkuu wa Anglikana duniani, Justin Welby (57), halafu Usiku saa 8-9 usiku Makanisa Mawili yanachomwa Donge Tanga, ina maanisha nini? Waharifu hawa si wanampuuza Rais? Awaadhibu!
Ni wakati muafaka sasa kwa Vyombo vya Usalama vimsaidie Rais aiaibishwe na mtu au Kukundi cha watu wachache, ambavyo mwenyewe amesema, Hatavivumilia na kwamba Serikali yake haitawavumilia watu wanaoendelea kuvuruga amani ya nchi kwa kisingizio cha masuala ya dini.
Nirejee moja ya Nukuu zake alizosema Dodoma katika hotuba yake, ambazo Polisi wakizitumia ni Meno ya kumsadia Rais, “Dini zote zinahimiza upendo, hakuna dini inayohubiri kuuana, ukiona dini inayohubiri kuuana hiyo itakuwa ni ya shetani, dini ya kweli inahimiza upendo kwa kila mtu,” alisema Rais Kikwete.
Hata hivyo Askofu Mkuu aliyewekwa wakfu, Dk Chimeledya hakunyamaza kimya, baada ya kutawazwa aliiomba Serikali kushughulikia changamoto za nchi ikiwamo suala la umaskini, maradhi, ujinga na hatari ya kuporomoka kwa Amani, ambapo alisema, Rushwa, Dawa za kulevya,Uufisadi naMauaji ya Vikongwe, ni miongoni mwa mambo yanayoiondolea sifa Tanzania ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikijulikana kama kisiwa chaAmani.
nyeregete@yahoo.co.uk 0715-933308
No comments:
Post a Comment