John Obi Mikel wa Nigeria (kushoto), akimtoka kiungo wa Taihiti katika mechi ya ufunguzi Kundi B la michuano ya Kombe la Mabara 2013. Katika mechi hiyo, Nigeria ilishinda mabao 6-1 na kuongoza kundi hilo linalojumuisha timu za Hispania na Uruguay.
Mfungaji wa mabao matatu 'hat-trick' Nnamdi Oduamadi, akimlamba chenga kipa wa Tahiti kuifungia Nigeria moja ya mabao hayo.
Wachezaji wa Nigeria wakimpongeza Oduamadi (wa pili kushoto) baada ya kufunga bao.
Ahmed Mussa wa Nigeria, akimpongeza Oduamadi baada ya kufunga bao.
Mshambuliaji Jonathan Tehau wa Tahiti, akipiga kichwa kufunga bao la kihistoria kwa nchi yake, wakati kikosi chake kilipolala kwa mabao 6-1 mbele ya Nigeria. Bao hilo ndio la kwanza kwa nchi hiyo kufungwa katika michuano ya kimataifa.
Wachezaji wa Tahiti wakishangilia bao la kihistoria katika mechi hiyo.
Wachezaji hao wakishangilia na kuwashukuru mashabiki waliojazana dimbani kwa kuwasapoti licha ya uchanga wao katika tasnia ya soka duniani.
RIO DE JANEIRO, Brazil
Kulikuwa na mashabiki 20,187 tu ndani ya dimba lililokarabatiwa la Estadio Mineirao, lakini wengi kama si wote walionekana kuisapoti Tahiti - nchi changa katika soka la kimataifa, ambayo nyota wake walijikusanya na kushangilia mwisho wa mchezo
MABAO matatu ‘hat-trick’ yaliyowekwa kimiani na mshambuliaji
Nnamdi Oduamadi, jana usiku yaliwawezesha Nigeria kuanza vema mechi za michuano
ya Kombe la Mabara kwa kuichapa Tahiti mabao 6-1 kwenye dimbala Belo Horizonte.
Mabingwa hao wa Afrika waliwasili Brazil saa 36 kabla ya
kuingia dimbani katika mechi hiyo, lakini hiyo haikuwazuia kukaa kileleni
katika kundi B linalowahusisha mabingwa wa Dunia Hispania – ambao pia
walishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Uruguay.
Ushindi huo wa Nigeria ulikuwa adhabu kubwa mno kwa Tahiti, inayokamata
nafasi ya 138 katiika viwango vya ubora duniani, lakini hakikuwafanya
kutoshangilia bao lao kwanza katika la kimataifa kwa nchi hiyo, lililofungwa
kwa kichwa na Jonathan Tehau.
Bao la Tehau mapema kipindi cha pili, lilikuja wakati ambao Nigeria
ilikuwa mbele kwa mabao 3-0, baada ya Elderson Echiejile kufunga la kuongoza
dakika ya tano na mawili ya Oduamadi katika dakika za 10 na 26.
Hata hivyo, Tehau akatibua sherehe yake robo saa baadaye,
kwa kujifunga kunako dakika ya 69, kabla ya Oduamadi na Echiejile kufunga
kunako dakika za 76 na 81 kukipa kikosi cha kocha Stephen Keshi ushindi muhimu
kuelekea mechi ya Ijumaa dhidi ya Uruguay.
Kulikuwa na mashabiki 20,187 tu ndani ya dimba lililokarabatiwa
la Estadio Mineirao, lakini wengi kama si wote walionekana kuisapoti Tahiti -
nchi changa katika soka la kimataifa, ambayo nyota wake walijikusanya na
kushangilia mwisho wa mchezo.
Supersport.com
No comments:
Post a Comment