HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 18, 2013

Kilimanjaro Premium Larger kuanza ‘Kili Music Tour 2013” kwa kishindo Dodoma!


Dar es Salaam, Tanzania, Juni 18, 2013:  Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya nembo yake  ya  Kilimanjaro  Premium  Lager,  inaanza  rasmi  tamasha  kubwa  la muzikilijulikanalo kama ‘Kili Music Tour’ wikiendi hii mjini Dodoma.


Tamasha kubwa  linatarajiwa  kuanza Jumamosi ya tarehe 22 Juni,  2013 mjini Dodoma kwenye viwanja vya Jamhuri na itajumuisha wasaniii 8 ambao ni Ally Kiba,   Ommy Dimpoz, Professor J, Ben Pol,  Lady Jay Dee, Lynex, Roma na Kala Jeremiah. 


Mwaka huu Kilimanjaro Premium Lager imedabilisha utaratibu wa tamasha hili la muziki ambalo lilikuwa linajulikana kama KTMA Winners Tour na lilikuwa likijumuisha wasanii walioshinda tuzo za Kili Tanzania Music Awards tu.

Mwaka huu bia ya Kilimanjaro imebadilisha jina la tamasha kuwa Kili Music Tour na litashirikisha wasanii wote kwa ujumla na sio washindi wa tuzo za KTMA tu.

“Kili Music Tour imepanua wigo wake kwa kushirikisha wasanii walioshinda tuzo, wasanii waliokuwa kwenye mapendekezo ya tuzo na wasanii ambao hawakushiriki kabisa kwenye tuzo lakini wako juu kwenye tasnia ya muziki nchini.

 Hii ni kwenye kuhakikisha kuwa mashabiki wa muziki wanapelekewa wasanii wanaowapenda kwenye mikoa yako bila kubagua. Mwaka huu matamasha yameongezeka kutoka sita mwaka jana na kuwa nane. 

Kili inaelewa ni jinsi gani watanzania wanajivunia mambo ya kitanzania  kama muziki wetu wa bongo flava, dansi yetu ya kiduku, kandanda letu lenye ushabiki wa simba na yanga, lugha yetu ya kipekee na bia yetu ya Kilimanjaro inayowapa bonge la kiburudisho .

 Ndio maana tumeongeza wigo wa Tamasha kama ishara ya shukurani kwa jinsi watanzania wanavyojivunia mambo ya kikwetu kwetu.” Alisema Bwana George Kavishe Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Msanii aliyebobea wa bongo flava ajulikanaye kama Kala Jeremiah naye alisema “ mwaka huu mashabiki wategemee kupata vionjo ambavyo hawajawai kuviona kwani mimi na wasanii wenzangu tumejipanga kikamilifu kuhakikish kuwa hatuwaangushi mashabiki wetu na kuwa tunawapa bonge la kiburudisho!”

No comments:

Post a Comment

Pages